Waasi wa Tuareg watangaza kujitenga na Mali
By Maganga Media - Apr 6, 2012
Waasi wa Tuareg wametangaza 'uhuru wa Azawad' na kujitenga eneo hilo na nchi ya Mali. Msemaji wa waasi hao Mossa Ag Attaher amewaambia waandishi habari kwamba, kuanzia leo wanalitangaza eneo la Azawad kuwa huru na kuongeza kuwa, waasi hao wataheshimu mipaka ya eneo hilo na nchi nyinginezo. Kundi hilo ni moja ya makundi makubwa mawili ya waasi waliozidisha shughuli zao baada ya serikali ya Mali kupinduliwa na jeshi hivi karibuni.
Hayo yanajiri huku Shirika la Msamaha Duniani Amnesty International likitahadharisha kuwa Mali inakabiliwa na hatari ya kupatwa na janga kubwa la kibinadamu kutokana na mapigano ya waasi. Jana pia Harakati ya Kupigania Kujitenga Azawadi (MNLA) ilitangaza kusimamisha mapigano nchini humo na kutaka eneo la Azawad litambuliwe na jamii ya kimataifa.
- Irib Swahili Service
- Irib Swahili Service
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII