HABARI MPYA LEO  

BAADA YA MAPINDUZI YA MALI

By Maganga Media - Mar 24, 2012

  • Uhalifu na wizi wa bidhaa wakithiri

  • Waasi wa Tuareg waendeleza mashambulizi Kaskazini mwa Mali.

  • Umoja wa Ulaya waiwekea vikwazo Mali

    Mapinduzi ya Mali


    Ikiwa leo ni siku ya tatu tangu jeshi la Mali lifanye mapinduzi, Kepteni Amadou Sanogo, kiongozi wa mapinduzi, ametokeza kwenye Televisheni ya taifa kuomba msamaha kwa wizi wa ngawira unaofanywa na wanajeshi wa daraja za chini, na wale aliowaita watu wasiokuwa na nia njema. Alisema vitendo hivyo siyo kazi wala azma yao. 

    Kepteni Sanogo piya alikanusha tetesi kwamba aliuliwa jana usiku, na kwamba njama nyengine ya mapinduzi inapikwa na wanajeshi watiifu kwa Rais Amadou Toumani Toure. Inaelekea maafisa wa vikosi vengine vya jeshi walikuwa wamemzunguka Kepteni Sanogo wakati wa hotuba yake hiyo kwenye televisheni, kuonesha kuwa jeshi liko pamoja na linaunga mkono mapinduzi hayo. 

    Inafikiriwa kuwa Rais Toure bado analindwa na kikosi maalumu na hakuna hakika kuwa jeshi zima sasa linamuunga mkono kiongozi mpya. Muungano wa vyama vikuu vya upinzani, umelaani mapinduzi hayo, na umetaka uchaguzi ufanywe. Uchaguzi ukitarajiwa kufanywa mwisho wa mwezi huu.

    MALI YAWEKEWA VIKWAZO
    Mawaziri wa Mambo ya Nje ya Umoja wa Umoja wa Ulaya wameiwekea vikwazo vya kiuchumi Mali kufuatia mapinduzi ya kijeshi ikiwa ni hatua mojawapo ya kushinikiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini humo. Uamuzi huo umefikiwa mjini Brussels kufuatia kikao kilichofanywa na mawaziri hao siku ya Ijumaa Machi 23 mwaka huu. Kwenye tamko lao la pamoja mawaziri hao wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya walilaani vikali kitendo kilichofanyywa na wanajeshi wa Mali na kuwataka kusitisha mapigano mara moja. 

    Tamko hilo pia limejumuisha amri ya kuwataka wanajeshi hao kuwaachia huru maafisa wa serikali wanaowashikilia akiwemo aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Amadou Touman Toure. Kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa nchini Mali, nimeamua kusitisha kwa muda shughuli zote za maendeleo zinazofanywa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini humo hadi hapo hali itakaporejea na kuwa kama inavyotakiwa." alisema Kamishna wa Masuala ya Maendeleo wa umoja huo Andris Piebalgs.

    Kikosi cha jeshi la waasi wa Mali


    Wakati vikwazo vya kiuchumi vikianza kuiandama Mali, huko Bamako mji mkuu wa nchi hiyo Kiongozi wa mapinduzi hayo kijeshi Kapteni Amadou Sanogo ametangaza mpango wa kuwapeleka mahakamani Rais wa nchi hiyo na viongozi wake wa juu ambao wanawashikilia hadi sasa. Pamoja na nia hiyo ya kuwafikisha katika mikono ya sheria viongozi hao, Kapteni Sanogo pia amezungumzia kuhusu usalama wa watu hao na kusema kuwa wako hai chini ya uangalizi mzuri.

    "Hawa watu wako salama salimini. Hatutawagusa hata nywele vichwani mwao. Nitawafikisha mahakani ili watu wa Mali wapate kuufahamu ukweli." Alisema Kapteni Amadou Sanogo katika mahojiano na Shirika la Habari la Ufaransa AFP katika kambi ya kijeshi karibu na mji mkuu wa nchi hiyo. Hata hivyo umoja huo umesisitiza kuwa bado utaendelea kuwasaidia raia wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa misaada ya moja kwa moja ya kibinaadamu. Mali inakabiliwa na tishio la baa la njaa kufuatia kukumbwa na ukame. Baraza la Umoja wa Ulaya lilipanga kutumia kiasi cha Euro milioni milioni 583 kwa ajili ya shughuli za maendeleo nchini Mali katika kipindi cha mwaka 2008 na 2013.

    mashambulizi zaidi

    Waasi wa Tuareg nchini Mali wameendeleza mashambulizi Kaskazini mwa nchi hiyo wakati huu ambapo askari hao waasi wanakosolewa na ulimwengu kwa kufanya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali kwa madai ya serikali kushindwa kumaliza mapigano nchini humo.

    waasi wa kundi la Tuareg waliofanya mapinduzi ya kijeshi nchini Mali
    waasi wa kundi la Tuareg waliofanya mapinduzi ya kijeshi nchini Mali

     Umoja wa Afrika AU umeisimamisha Mali kwa muda katika umoja huo, wakati Ulaya imesitisha misaada na Marekani imetishia kufanya hivyo huku kukiwa na mfululizo wa matamko ya kukosoa mapinduzi hayo ya kijeshi katika nchi hiyo kinara katika mapambano ya usafirishaji wa dawa za kulevya.
    Mapinduzi hayo yamefungua njia kwa waasi hao wa Tuareg kuimarisha udhibiti wa eneo la Kaskazini huku kundi lao la harakati za kitaifa za ukombozi wa Azawadi MNLA likisema kuwa wameuteka mji wa Anefis ulioko katikati mwa miji muhimu ya Gao na Kidal.


    Maganga Media

    Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

    ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII