HABARI MPYA LEO  

Ureno, Ujerumani zatinga robo fainali

By Emmanuel Maganga - Jun 18, 2012

Ureno

Cristiano Ronaldo aliiwezesha Ureno kuingia robo fainali

Mabao mawili ya mshambulizi Cristiano Ronaldo yaliiwezesha Ureno kuingia robo fainali ya michuano ya Euro 2012, kwa kuifunga Uholanzi, na pasipo shaka yoyote, kuwalazimisha kurudi nyumbani.

Kwa Uholanzi kuwa na matumaini yoyote kuendelea kusalia katika mashindano hayo, walilazimika kuifunga Ureno magoli 2-0, na bao la kwanza la mkwaju wa kupinda kutoka kwa Rafael van der Vaart liliwapa matumaini Uholanzi walipoweza kutangulia.

Lakini mchezo wa Uholanzi uliendelea kufifia, na Ronaldo alifanikiwa kusawazisha, alipopigiwa mpira na mwenzake Joao Pereira.

Nani alimsaidia Ronaldo kufunga kwa mara ya pili, na Ureno ikavuka hatua ya makundi na kujiandikishia nafasi katika robo fainali.

Ureno sasa itacheza na Jamhuri ya Czech, inayoongoza kundi A.

Ujerumani yafuzu kwa robo fainali

Ujerumani

Mashabiki wengi wanaifikiria timu ya Ujerumani imo katika nafasi nzuri ya kuwa bingwa Euro 2012

Lars Bender alifunga bao la ushindi la Ujerumani siku ya Jumapili zikiwa zimesalia dakika 10 kabla ya kipenga cha mwisho, na kuiwezesha nchi yake kuwa miongoni mwa nchi nane ambazo zitashiriki katika michuano ya robo fainali.

Bender, mwenye umri wa miaka 23, na ambaye ni mchezaji wa Bayer Leverkusen ya Ujerumani, aliizima ndoto ya Denmark ya mwaka 1992, walipowashinda Wajerumani katika fainali.

Ujerumani iliweza kuongoza katika mechi hiyo dakika ya 19 wakati Lukas Podolski alipofunga, lakini Michael Krohn-Dehli aliweza kuisawazishia Denmark dakika sita baadaye na kuipatia nchi yake matumaini ya kufika robo fainali.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII