Mapacha waahidi kumsaidia dogo Janja apate haki zake
By Unknown - Jun 18, 2012
Kundi la Hip-hop linaloundwa na mapacha K na D wa Maujanja Saplayaz limeahidi kufanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa Diogo Janja aliyefukuzwa Tip Top Connection na kurudi Arusha wiki hii anapata haki yake. Kulwa ambaye ni mmoja wa mapacha hao amesema sio haki msanii huyo mwenye umri mdogo kurudi nyumbani bila chochote licha ya kuliingizia kundi hilo hela fedha za kutosha kutokana na show alizokuwa akifanya.
“Haki ya Dogo Janja iko wapi? Kama anarudi Arusha bila ya chochote! Madee imefika mahali lazima watu wajue ukweli maana maongezi yako kwenye vyombo vya habari yanagongana. Kama kuna unyonyaji ulikuwa unaendelea basi watanzania wajue na hatma ya huyo dogo ifikiwe na apewe haki yake. Tumeshoshwa na unyonyaji magenge ya mwenge,” aliandika K kupitia Facebook wiki hii.
Dogo Janja alirudi kwao Arusha Alhamis ya wiki hii baada ya uongozi wa Tip Top Connection kusema kuwa alilewa sifa, kuendekeza starehe na utoro shuleni. Hata hivyo yeye alisema ameamua kuondoka baada ya kuishi maisha ya tabu, kudhulumiwa haki yake na kufanywa kama kitega uchumi cha kundi hilo.
Akiongea kwa huzuni baada ya kuulizwa ni kiasi gani cha pesa amewahi kulipwa kutokana na mauzo ya Album yake, Dogo Janja kasema “Eeeeeeehh bro nikizungumzia swala la Album yani daaaaaaahhhhhh, nakumbuka kuna kipindi nilitaka kuliongelea nikawekwa chini nikaambiwa usiliongelee sasa sijui kama ni yule Muhindi au ni Madee, album iliuzwa kwa Muhindi na nilisaini mkataba na kupiga picha za Album ikatoka lakini ile album kiukweli hata ukinipa msaafu sasa hivi nashika, sijawahi kula shilingi tano yangu ya album mi namwachia mwenyenzi Mungu mpaka Madee aliniambia wewe ukiulizwa kwenye Radio sema ile album uliifanya kwa kumbukumbu tu hata ukija kuzeeka utakuja kuwaambia wajukuu zako nilifanyaga album ya Mtoto wa Uswazi ilikua na nyimbo tisa lakini usiitolee macho album haina hela”
“Naapa kwa mwenyenzi Mungu kama nimekula hata shilingi kumi yake nife hata sasa hivi yani, mpaka ilifikia kipindi nikienda kufanya show Mwanza nakwenda kwa Mamu nanunua kopi zangu 20, album niliuza bure mimi nikawa nanunua kwa shilingi elfu mbili pale dukani Umoja, nikifika mikoani ndio nauza CD moja labda shilingi elfu 5 napiga sign watu wanakuja wananunua, kihalali ile Album sikunufaika nayo chochote, wamenufaika nayo watu” – Dogo Janja.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII