March 13, 2025
 

HABARI MPYA LEO  

NAFASI ZA KAZI

SENIOR PLANNING OFFICER      Qualifications: Bachelor’s Degree in Economics, Statistics, Planning, Bu...

Published by Admin

ACADEMIC NEWS AND SELECTION

TUMAINI UNIVERSITY MAKUMIRA (TUMA) FIRST LIST OF ADMITTED STUDENTS INTO VARIOUS PROGRAMMES AT (TUMA) 2012- 2013 INTAKE 1. Th...

Published by Admin

MAKALA MBALIMBALI

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

Published by Admin

MICHEZO NA BURUDANI

Mshambulizi wa timu ta taifa ya soka ya Uganda Cranes, Uganda, Robert Ssentongo, ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mashindano y...

Published by Admin

Makundi ya timu Kagame kujulikana leo!

By Unknown - Jun 30, 2012

WAPINZANI wa Yanga, mabingwa watetezi Kombe la Kagame watajulikana leo wakati ratiba ya michuano hiyo itakapowekwa hadharani tayari kwa michuano hiyo itakayoanza Julai 14 hadi 28 kwenye Uwanja wa taifa, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, Cecafa, Nicholaus Musonye alisema jana kuwa ratiba hiyo itakuwa hadharani baada ya timu zote kuthibitisha kushiriki michuano hiyo.

Yanga inayotetea ubingwa wake, huenda ikafungua dimba la michuano hiyo. Itasindikizwa na timu za Simba (bingwa Bara) na Azam iliyoshika nafasi ya pili. Musonye alisema kuwa michuano itafanyika kama ilivyopangwa jijini Dar es Salaam na ule wa Azam wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 7,000.

Timu zitakazoshiriki ni APR (Rwanda), Yanga, Simba, Azam (Tanzania), Tusker (Kenya), Wau Salam (Sudan ya Kusini) na Atletico ya Burundi. Timu nyingine ni Mafunzo (Zanzibar) Mamlaka ya Mapato (Uganda), Elman (Somalia), Ports (Djibouti), Red Sea (Eritrea) na Coffee ya Ethiopia.

Naye Rais wa Cecafa, Leodegar Tenga wamemshukuru Rais Paul Kagame kwa jitihada zake za kuinua soka katika ukanda huo. Rais Kagame amekuwa akidhamini michuano ya Cecafa tangu 1999. Musonye aliwataka wadhamini wengine kujitokeza kusaidia kufanikisha michuano ya 2012 kama ilivyofanya Supersport ambayo imeahidi kuonyesha 'live' mechi za michuano hiyo.

Wakati huo huo, Dynamos ya Zimbabwe imetupilia mbali mwaliko wa Cecafa kushiriki michuano yake kwa kuwa inajiandaa na mechi za Kombe la Caf dhidi ya Inter-club ya Angola.

Dynamos itacheza mechi yake kati ya Julai 14 na 16 siku ambayo michuano itaanza. Mbali na mechi hiyo, pia inakabiliwa na mechi ya ligi dhidi ya Hwange na Highlanders pamoja na michuano ya Banc ABC Super Eight inayoanza Julai 21.

Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Ray Kazembe alisema kuwa hawataweza kwenda Tanzania kutokana na majukumu hayo. Mbali na timu hiyo, Musonye alisema pia kuwa wanatarajia Vita Club ya DRC pamoja na Bloemfontein Celtics, Platinum FC na Silver Stars za Afrika Kusini kushiriki michuano hiyo.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII

Pages 22123456 »