HABARI MPYA LEO  

Boko Haram kupatanishwa na serikali

By Maganga Media - Jun 7, 2012

Kiongozi mmoja wa kidini nchini Nigeria amesema kuwa anaongoza mazungumzo ya upatanishi kati ya wapiganaji wa Boko Haram na serikali ya jimbo. Sheikh Dahiru Bauchi amesema kuwa pande hizo mbili zimekubaliana kuanzisha mazungumzo juu ya namna ya kumaliza harakati za kundi hilo haramu.
Sheikh Dahiru ataka kukomesha viliyo

Taarifa ya Sheikh Dahiru Bauchi inatokea wakati kukiwa na uhasama baina ya vikosi vya usalama nchini Nigeria na kundi la Boko Haram. Tangu siku ya jumapili kumekuwepo na mashambulio mapya yanayofanywa na kundi hilo na vikosi vya usalama vinasema kua vimewaua wapiganaji 16 wa kundi hilo hapo jana jumanne.

Sheikh Dahiru ndiye kiongozi wa kundi la Kiislamu la Tijjaniyya mojawapo ya makundi makubwa ya Kiislamu nchini Nigeria.
Boko Haram
Boko haram
Ingawa Boko Haram si sehemu ya kundi hilo, kiongozi huyo anaheshimiwa mno kama msomi katika dini ya Kiislamu. Aliongeza kusema kua ana idhini ya uongozi wa makundi yote pamoja na wakuu wa serikali ya Nigeria bkuanzisha mchakato wa amani.
Alisema pia kua Boko Haramu limeitaka serikali iwaandikie barua Boko Hamaramu kama mwaliko wa kushiriki mazungumzo yab amani. Serikali ya Jimbo la Bauchi imekiri kua ilihusika katika juhudi za kuandaa mazungumzo hayo kwa niaba ya serikali kuu ya Nigeria.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII