Marekani kuendelea kutumia ndege zisizo na rubani Pakistan
By Maganga Media - Jun 7, 2012
Alitoa matamshi yake wakati akihudhuria mkutano katika nchi jirani ya India. Hapo jana Pakistan ilimtaka balozi wa Marekani nchini humo kuelezea tena wasiwasi wa Pakistan kuhusiana na matumizi ya ndege hizo dhidi yake. Ndege nane kama hizo zimeshambulia maeneo ya wanamgambo nchini Pakistan katika wiki mbili zilizopita licha ya serikali ya Pakistan kutaka Marekani kukomesha mashambulizi hayo.
Kwa upande wake Pakistan inasema kuwa mashambulizi kutumia ndege hizo, yanachochea hisia zaidi za chuki dhidi ya Marekani na inadai kuwa raia wasio na hatia wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo.
Hata hivyo Marekani inasisitiza kuwa mashambulizi hayo yamekuwa na faida kubwa katika vita vyake dhidi ya Al Qaeda hususan katika eneo lenye wanamgambo la mpakani mwa Pakistan na Afghanistan. Maafisa wa Marekani wanasema kuwa kiongozi wa Al Qaeeda Abu Yahya al-Libi, alifariki katika shambulizi la makombora mawili katika mojawapo ya makazi ya wanamgambo mashariki mwa mji wa Miranshah.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII