HABARI MPYA LEO  

Nsajigwa atemwa Kagame

By Unknown - Jul 13, 2012


SIKU za nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa kuendelea kuichezea klabu hiyo zimeanza kuhesabika baada ya jana kuenguliwa kwenye kikosi cha wachezaji 20 wa kocha Tom Saintfiet kitakachoshiriki Michuano ya Kagame.

Uamuzi huo wa Saintfiet ni pigo jingine kwa Nsajigwa ambaye hivi karibuni aliliripotia kutaka kuachwa na mabingwa hao kutokana na kushuka kiwango, pia alidai kuhusika katika kusababisha Yanga kufunga 5-0 na Simba mwishoni mwa msimu uliopita.

Akizungumza na Wanahabari kocha Saintfiet alisema hakumjuisha Nsajigwa kwenye kikosi hicho kwa lengo la kumpatia muda wa kutosha wa kupumzika na awe tayari kwa kuitumikia timu hiyo katika Ligi Kuu hapo baadaye.

"Nsajigwa ni mchezaji mzuri, lakini nimeamua kumpumzisha kwenye michuano hii kwa sababu msimu uliopita alicheza mechi nyingi na sasa anahitaji kumpumzika ili awe tayari kwa Ligi Kuu.

“Sababu nyingine iliyonifanya nichukue uamuzi huu ni kwamba katika nafasi yake kuna wachezaji wengi vijana walioonyesha soka ya kiwango cha juu, hivyo nataka kuwapa uzoefu wa kutosha wa mechi za kimataifa," alisema Saintfiet.

Wachezaji wapewa nafasi ya kurithi namba ya Nsajigwa kwenye michuano ya Kagame ni David Luhende, Juma Abdul, Oscar Joshua, na Godfrey Taifa.

Nahodha huyo wa Yanga alianza kupata pigo msimu huu baada ya kuumia mwezi Oktoba 2011 na kushindwa kuichezea Taifa Stars katika mchezo wake dhidi ya Morocco wa kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 2012. Pia, alivuliwa unahodha wake kwenye kikosi cha Stars kinachonolewa na kocha Kim Poulsen.

Mbali ya Nsajigwa wachezaji wengi wa Yanga walioachwa na kocha Saintfiet ni pamoja na majeruhi Nurdin Bakari na kiungo chipukizi Frank Domayo, Simon Msuva na Omega Seme wanatumia timu ya taifa ya Vijana iinayojiandaa na mechi za kimataifa dhidi ya Rwanda na Nigeria.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII