HABARI MPYA LEO  

KIJIJI CHA WIKI: IFAHAMU NG'ONG'ONA

By Maganga Media - Apr 19, 2012


Karibuni katika safu mpya inaitwa maisha halisi ya Mtanzania. Katika safu hii tutakuwa tunatembelea vijiji vyetu kujionea hali halisi. Leo tupo katika kijiji cha Nghong'onha ambacho wengi wenu mmezoea kukiandika Ng'ong'ona.

Safari yetu ya leo ilikuwa ni kutembelea kijiji cha Nghong'ona kijiji maarufu sana hapa mjini Dodoma. Kipo Manispaa ya Dodoma mjini nje tu kidogo ya mji, chini ya Chuo kikuu cha Dodoma kitivo cha Elimu. Ukiwa kijijini hapo utajionea mambo mengi tu mazuri na ya kuvutia. Wakazi wake wanafurahia sana uwepo wa UDOM na kwa hakika hicho ndio pekee kinachowasaidia katika maisha yao ya kila siku.

KILIMO CHA ALIZETI
Hili ni miongoni mwa mashamba ya zabibu, matunda maarufu mkoani Dodoma
Kilimo cha Mahindi pia kinakubali
Wakazi wa kijiji hicho ni wakarimu kweli. Tuliokutana nao wanatoka shamba hawakusita kutukaribisha karanga walizovuna hata bila kuwaomba. Na pindi inapotokea mnajua lugha yao na kuwasalimia hufurahia sana na kujiona kuwa umewaheshimu sana.
Vijana wakila karanga walizopewa
Kijana akila Karanga

Mazao mengine yanayopatikana kwa wingi kijijini hapo ni pamoja na Karanga, mtama, uwele, maboga, nk.
Bonde hili ni la ajabu kidogo, Ndio sehemu wanayochota maji ya matumizi. Wakitaka maji wanafukua chini kidogo tu kisha wanachota kwa bakuli hadi wanajaza vyombo vyao. Ni mkondo wa maji kutiririka kutoka milimani wakati wa masika
Hapo ndio maji yanapotoka baada ya kufukua
Dogo ametoka kuchota maji

Dogo ametoka kuchunga ng'ombe
Wanafunzi wametoka shule
Biashara ya mawe pia kwa sana
Ujenzi wa makazi mapya unaendelea kufuatia kijiji kukua kwa haraka sana baada ya kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Dodoma. Baadhi ya wanachuo wamepanga huku baada ya kuwa ama wameoa au wananyonyesha kwani sheria za chuo haziruhusu mtu kukaa Hosteli akiwa na mtoto au ana mke.
Misosi pia inapatikana kwa wingi na bei nafuu
KITUO CHA BIASHARA NDOGO NDOGO KIJIJINI HAPO











Kama kawaida ya vijiji vyetu, huduma ya vyoo ni lazima upite msitu huo uliopo nyuma ya nyumba

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII