HABARI MPYA LEO  

Simba yatwaa ubingwa Kombe la Urafiki!

By Unknown - Jul 13, 2012

SIMBA SC imechukua ubingwa wa Kombe la Urafiki, baada ya kuifunga Azam FC kwa penalti 3-1 usiku huu kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kutokana na sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.

Uhuru akiwa na Boban baada ya ushindi, Boban alikosa penalty.

.

.

.

.

.

Penalti za Simba ziliwekwa ndani na Mwinyi Kazomoto, Amir Maftah na Kiggi Makassy, wakati Haruna Moshi Boban alipaisha na kwa upande wa Azam FC, aliyefunga ni Hamisi Mcha ‘Vialli’ pekee, wakati ya Samir Hajji Nuhu ilidakwa na Juma Kaseja, Ibrahim Mwaipopo ilipanguliwa na Himid Mao ‘iliota mbawa’.

Kabla ya matuta, mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia Felix Sunzu alitangulia kuifungia Simba dakika ya 29 kabla ya Hamisi Mcha ‘Vialli’ kusawazisha dakika ya 45 na ushei, Kipindi cha pili mchezo ulichangamka zaidi na dakika ya 81, John Bocco ‘Adebayor’ aliyetokea benchi aliifungia Azam bao la pili, kabla ya Kazimoto kuisawazishia Simba kwa penalti dakika ya 87, baada ya Danny Mrwanda kuangushwa kwenye eneo la hatari ambapo kwa ushindi huo, Simba SC wamezawadiwa Sh. Milioni 10 na Azam FC Milioni 5.

.

.


(Stori na picha vyote vimeandaliwa na BIN ZUBERY wa bongostaz.blogspot.com)

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII