Mshambulizi wa timu ta taifa ya soka ya Uganda
Cranes, Uganda, Robert Ssentongo, ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa
mashindano ya CECAFA Tusker Senior Challenge Cup, yaliyomalizika mjini
Kampala.
Sentongo hata hivyo alifunga magoli manne pekee wakati wa mashindano hayo.
Wachezaji waliofunga idadi magoli mengi kuliko Sentongo,Mrisho Ngassa na John Bocco wa timu ya Tanzania bara, walinyimwa tuzo hilo, na kamati ya ufundi ya mashindano hayo.
Katika mashindano yaliyopita, mchezaji aliyefunga idadi kubwa ya magoli ndiye huibuka mshindi wa taji hilo, lakini mwaka huu mambo nchini Uganda yalikuwa tofauti.
''Ngassa
na Bocco walifunga magoli matano kila mmoja na ilitarajiwa wangepewa
tuzo ya mfungaji bora lakini katika hali ya kushangaza kamati ya CECAFA,
ilimpa tuzo hilo mshambuliaji wa Uganda, Robert Ssentongo aliyefunga
magoli manne'' Alisema kocha wa Kilimanjaro Stars.
Katibu mkuu wa CECAFA akiwa na kome la CECAFA Senior Challenge
Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti ya mwamuzi wa
mechi ya fainali kati ya Uganda Cranes na Kenya, Ghiery Nkurunziza
kutoka Burundi, Sentongo ndiye aliyefunga bao la ushindi la Uganda,
lakini kuna habari za kutatanisha kuwa, bao hilo lilikuwa la kujifunga.
Hata hivyo, ushahidi wa picha za televisheni
unaonyesha kwamba beki wa Kenya, Anthony Kimani, alijifunga magoli yote
mawili ya fainali.
Baada ya mechi hiyo ya fainali, kipa wa Harambee
Stars Duncan Ochieng anaripotiwa kughadhabishwa sana na kitendo hicho
cha Kimani kiasi cha kutaka kupigana na beki huyo, kwa kusababisha Kenya
kupoteza Kombe hilo.
Wengine waliotuzwa baada ya mashindano hayo ni
pamoja na Brian Umony, ambaye alitangazwa kuwa mchezaji bora, Hamza
Muwonge kutoka Uganda naye aliibuka Kipa bora baada ya kufunga bao moja
pekee wakati wa mashindano hayo.

Moja ya vitu vinavyoashiria ubora zaidi wa shindano hilo kwa mwaka huu kulinganisha na mashindano ya miaka iliyopita, ni mjengo ambao unawahifadhi washiriki wote katika kipindi chote cha shindano hilo, mpaka siku atakapopatikana mshindi wa zawaidi kubwa ambayo ni Million 50 tsh.
HUKU wadau wakiwa na shauku kubwa ya kumjua mshindi wa shindano hili la kumsaka staa wa kike mwenye mvuto ambaye hajaolewa ‘The Ijumaa Sexiest Girl’, hatimaye kura za wasomaji zimeamua msanii wa filamu, Jackline Wolper kutoa mkono wa kwaheri.
Mratibu wa shindano hili, Imelda Mtema alisema: “Mtifuano ulikuwa mkali sana na hii ilitokana na ukweli kwamba, wote waliobaki ni wakali kuanzia sura hadi maumbo yao. Wopler ametolewa na sasa kimbembe ni kati ya Wema na Agnes.”
Kufuatia matokeo hayo ya Wolper kuchapa lapa, sasa wanabaki Wema na Agnes ambao watapigiwa kura kwa wiki mbili kabla ya kumpata mshindi. Ili kushiriki katika hatua hii muhimu ya kumpata mshindi, andika jina la mshiriki kisha litume kwenda namba 0786-799120.
Beki wa kimataifa wa Yanga Mbuyu Twite akionesha jezi namba 4 aliyovikwa na mashabiki wa Yanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege leo. Jezi hiyo ambayo imeandikwa 'RAGE' ni jina la Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage inanokana ni kijembe kwa mahasimu hao wa Yanga ambao awali walitangaza kumsajili kwa dau la dola 30,000 kabla ya Yanga kumpandishia hadi dola 50,000.
Hapa Twite akivishwa jezi hiyo yenye jina la Rage na mwanachama maarufu wa Yanga
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA SPORTS LADY, Dina Ismail

Hivi karibuni mwanamuziki wa kike wa nchini Tanzania, Rehema Chalamila aka Ray C amerejea nchini baada ya kukaa Nairobi, Kenya kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Alipozungumza hivi karibuni baada ya kufika, mrembo huyo alisema anahitaji mume wa maana ambaye atamuoa.
“Sina mume wala mpenzi, kwa sasa nipo single, ukiniulizia ishu za zamani ntakushangaa kweli, vigezo ndiyo hivyo, kama kuna mtu yupo tayari ajitokeze tufunge ndoa,” alisema Ray C.
Aliongeza kuwa akimpata mume huyo yupo tayari kumzalia watoto wawili na amechoka na maisha ya usela na kuwa na mahusiano na watu maarufu.
Wanaume wa Kenya wamekisikia kilio chake na wamewasiliana na mtandao wa Daily Post wa Kenya kumwambia Ray C watampa penzi moto moto.
“Ray C if u wish 2 huk up wit mi,take tiz no.0702868104, I’m in Thika central Kenya.”
“Hey somebody hook me up with the gal”
“She is a super hot chick !! What’s her email ? Lets hook up!”
“I am here to satisfy your needs”
“d.mokoro@yahoo.com.she can reach me, I also need a wife seriously”
“Rehema Chalamila contact me at danielluke76@gmail.com”
“Yes I can got me on diemoadish@gmail.com please”
“Come Baby come!”
“She is a very awesome lady n av always liked her. We all have past’s n it’s not something to keep on holding to … I am interested in her, to ask her out. I think she’s a good lady.”
“Ray C, if you come across this, reach me on wilnj85@gmail.com”
Katika hatua nyingine mtandao huo umesema kulikuwa na tetesi kuwa mhasibu wake nchini Kenya alimuibia pesa zake zote na hivyo akajikuta akishidwa kumudu maisha kwenye maeneo ya kifahari na hivyo kuhamia South B ambako alikuwa akiishi maisha ya kawaida.

Safari ya Prezzo nchini Nigeria imemrudisha bila kukipata kile alichokiendea baada ya Goldie kuonekana kutofurahishwa na ziara yake.
Prezzo aliyekuwa mshindi wa pili kwenye Big Brother Africa StarGame wiki hii alienda nchini Nigeria kuwaomba radhi wananchi wa huko na pia kutangaza nia ya kumfanya Goldie awe mke wake.
Katika mahojiano na waandishi wa habari jijini Lagos, Prezzo alisema alienda nchini humo kumuomba uchumba Goldie.
Hata hivyo hakufanikiwa kuonana Goldie ambaye Prezzo alisema hakuwa anapokea simu yake.
Hadi leo Goldie hajazungumzia chochote kuhusu ziara ya Prezzo.
Shabiki mmoja kupitia Twitter alimuuliza Goldie “Good afternoon madam, is it true that Prezzo is in town?” na yeye kumjibu “I also heard the pope is catholic. Is it true?”
Baadaye aliandika, “Gone R d days wen a problem shared is a problem solved; nowadays a problem shared becomes a topic of discussion. So keep ur problems 2urself!”
Kisha kuongeza: “Any1 can say anything, after all talk is cheap. But it’s in ur ACTIONS dat we’ll C ur tru intentions&where ur heart lies.”

Baada ya muigizaji mkongwe Hashim Kambi kuanza kutayarisha filamu zake mwenyewe, Jackline Wolper naye ameunga tela.
Muigizaji huyo mrembo amesema kupitia kampuni ya JB Production, ataanza kuandaa filamu zake.
Katika azma hiyo, Wolper atasaidiwa na meneja wake Leah Mwendamseke aka Lamata.
Vyanzo vimedai kuwa tayari kampuni hiyo imekamilisha kurekodi filamu iitwayo Malipo ni Hatari.
“Nimeingia katika fani ya utayarishaji na kwa kuanza ninakuja na filamu ya Malipo, ni filamu ya kipekee kuanzia hadithi, waigizaji wake wameigiza katika kiwango kikubwa cha kimataifa , okay sisemi mengi bali mtaona katika filamu ya Malipo,” Jack aliuambia mtandao wa FC.
Miongoni mwa waigizaji walioshiriki kwenye filamu hiyo ni pamoja na yeye mwenyewe, Blandina Chagula ‘Johari’, Stanley Msungu ‘Seneta’, Hashim Kambi ‘Ramsey’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’, Mgata, Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo, Slim na wengine.
Malipo ni Hatari imeongozwa na Lamata.
Muigizaji huyo mrembo amesema kupitia kampuni ya JB Production, ataanza kuandaa filamu zake.
Katika azma hiyo, Wolper atasaidiwa na meneja wake Leah Mwendamseke aka Lamata.
Vyanzo vimedai kuwa tayari kampuni hiyo imekamilisha kurekodi filamu iitwayo Malipo ni Hatari.
“Nimeingia katika fani ya utayarishaji na kwa kuanza ninakuja na filamu ya Malipo, ni filamu ya kipekee kuanzia hadithi, waigizaji wake wameigiza katika kiwango kikubwa cha kimataifa , okay sisemi mengi bali mtaona katika filamu ya Malipo,” Jack aliuambia mtandao wa FC.
Miongoni mwa waigizaji walioshiriki kwenye filamu hiyo ni pamoja na yeye mwenyewe, Blandina Chagula ‘Johari’, Stanley Msungu ‘Seneta’, Hashim Kambi ‘Ramsey’, Fatuma Makongoro ‘Bi. Mwenda’, Mgata, Ahmed Ulotu ‘Mzee Chilo, Slim na wengine.
Malipo ni Hatari imeongozwa na Lamata.

Maisha Plus is back na shughuli ya kusaka washiriki wa kuingia kijijini mwezi October utaanza rasmi siku ya Jumatatu ijayo kwa ajili ya usaili.Tofauti na usaili wa mashindano yaliyopita, vijana hao 26 watatafutwa katika vijiji ambavyo Mama Shujaa wa chakula wapatao 15 walipatikana kutokana na mchakato uliofanywa na shirika la chakula na kilimo la Uingereza la Oxfam ambalo msimu huu litashirikiana na waratibu wa shindano hilo.
“Vijana wa Maisha Plus wataingia kijijini, watakwenda kuchanganyika na hao kinamama, watakaa kwa siku tatu jumla kwa maana ya kwamba watakaa siku 12, 13 na siku 14. Katika hizi siku tatu vijana watakapochanganyika na hawa akinamama mle ndani tutatengeneza makundi ambapo kila mama mmoja mzalishaji wa chakula atakuwa na timu ya vijana tuseme watatu, wanne, sita kulingana na idadi ya washiriki wa Maisha Plus ambayo mwaka huu imeongezeka kutoka 18 hadi 26", Masoud Kipanya ambaye ndiye mratibu wa shindano hilo.
Mshindi wa mwaka huu atakamata kitika cha shilingi milioni 20.

Suma Mnazaleti na aliyekuwa meneja wa Mtanashati Entertainent, Maneno wamefukuzwa Mtanashati Entertainment kutokana na kuonesha utovu wa nidhamu.
Akiongea na Clouds FM kwenye 255 ya XXL leo, mkurugenzi wa kampuni hiyo Ustaadh Juma amesema meneja huyo amekuwa akitumia cheo chake vibaya na pia kuwa na tabia ya kutoa siri za kampuni.
Amesema zaidi ni jana kwenye fainali za kipindi cha Bibi Bomba baada ya meneja huyo kushindwa kufanya kazi yake inavyotakiwa ya kuwaangalia wasanii wake ambao jana walilewa kiasi cha kuiabisha kampuni yake.
Amesema Suma Mnazaleti amekuwa na tabia chafu kiasi cha kuwaharibu wasanii wake ambapo PNC alikuwa ameacha kunywa pombe lakini tangu Suma ajiunge nao, PNC amerudia kunywa pombe.
Hata hivyo Meneja Maneno ambaye naye amehojiwa amedai kuwa yeye ndiye ameacha kazi baada ya kuona ubabaishaji mwingi kwenye kampuni hiyo.
"Baada ya party ya Bibi Bomba, wasanii wote wametembea kwa mguu wengine mpaka Mwenge, yeye keshachomoka, alichokifanya ni kumchukilia tu Taxi Dogo Janja, halafu leo hii unaondoka unasema wewe ni mtanashati," alisema.
"Meneja huna hata shilingi kumi, unabeep unafanya nini, kwanini nisifanye kazi zangu binafsi. Mimi ndo nimekataa na nimeikataa hiyo Mtanashati lakini naweza nikakuonesha meseji , mimi ndo nimemwambia sitaki sio kwamba yeye ndio kanitumia, hana uwezo wa kunitumia yule mimi."
Yanga imewasili Kigali Rwanda kwa mwaliko wa rais Paul Kagame.
.
.
.
-
Truvada is already used in combination with other drugs to treat HIV-positive patients Continue reading the main story Re...
-
Kuna habari za sasa hivi meli iliyokuwa imebeba abria zaidi ya 200 ikitoka Dar kwenda Zanzibar imezama muda si mrefu,chanzo breaking ne...
-
MONUSCO peacekeepers on patrol. UN Photo/Sylvain Liechti 6 July 2012 – Expressing concern over the situation in the eastern Democratic Repub...
-
Mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari Tanzania Dr Steven Ulimboka aliyekuwa nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya matibabu baada ya kutekwa, ...
-
Bado mpaka sasa kumbukumbu za watanzania hazijalala, movie star marehemu Steven Kanumba bado anakumbukwa kwa sababu bado kazi zake nying...