HABARI MPYA LEO  

Tetemeko la ardhi laua mamia Iran

By Mhariri - Aug 12, 2012

Iranians search for survivors under the rubble of houses in the town of Varzaqan some 60 kms northeast of Tabriz (AFP Photo / Mahsa Jamali)
Idadi ya watu waliokufa kwenye mitetemeko miwili ya ardhi nchini Iran inazidi kuongezeka, na sasa inajulikana kuwa watu kama 250 wamekufa. Shughuli za uokozi baada ya mitetemeko ya Iran huku Watu wengine 2,000 wamejeruhiwa.

Vikosi vya waokoaji wanawatafuta walionusurika kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka katika miji na vijiji kwenye eno la mji wa Tabriz, kaskazini-magharibi mwa nchi.

Shirika la Mwezi Mwekundu la Iran limechukua uwanja wa mpira kuwapa hifadhi watu waliopoteza makaazi yao, au wanaogopa kurudi nyumbani. Shirika hilo limetoa mahema, mablanketi na chakula. Shirika la Mwezi Mwekundu la Uturuki, limesema linatuma msaada mpakani.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII