HABARI MPYA LEO  

Mkuu wa Olimpik Morocco kukamatwa

By Mhariri - Aug 4, 2012

Jenerali Housni Benslimane atakikana na polisi Ufaransa
Jaji mmoja nchini Ufaransa amewaomba polisi wa Uingereza wamkamate kiongozi wa ujumbe wa Olimpik wa Morocco ambaye kwa sasa yuko jijini London. Kiongozi huyo wa Olimpiki Jenerali Housni Benslimane,anadaiwa kuhusika na kutoweka kwa kiongozi wa upinzani wa Morocco Bwana Mehdi Ben Barka.
Mwanasiasa huyo wa upinzani wa Morocco wa alitoweka mwaka 1965 akiwa Ufaransa. Jaji Patrick Ramael tangu mwaka wa 2007 amekuwa akitaka Housni Benslimane akamatwe. Jaji huyo amekuwa akitaka kiongozi huyo wa Olimpik na wanajeshi watatu wa zamani wa Morocco wahijiwe kutokana na kutekwa nyara kwa Bwana Ben Barka mjini Paris. Lakini ubalozi wa Moroccan mjini London unasema kuwa Jenerali Benslimane alikuwa jijini humo wiki iliyopita lakini ameshaondoka.

Ingawa Jaji Ramael alitoa waranta yakutaka kiongozi huyo wa Olimpiki akamatwe miaka saba iliyopia lakini haitambuliki kwa sababu hadi sasa polisi wa kimataifa Iterpol na wakuu wa mashitaka nchini Ufaransa bado hawajaikubali.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII