Mahafari za Milambo Sec enzi hizo.
By Mhariri - Aug 12, 2012
Hii ni moja ya mahafari yaliyowahi kufanyika shuleni Milambo. Ilikuwa mwaka 2003.
Wa kwanza kulia ni aliyekuwa mkuu wa shule hiyo, Mohamedi Majubwa, anayefuatia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi, akifuatiwa na aliyekuwa makamu mkuu wa shule Mwl Rwabukoba (saizi ni Marehemu) na mwisho kabisa ( Waliosimama) ni mwalimu Camerius, aliyekuwa mwalimu wa Taaluma saizi ni mkuu wa shule. Kama macho yako bado yanaona vizuri anayefuatia ni mwalimu Kwigeza. Hapo ni nje ya bwalo la shule hiyo, usiulize upande waliokaa wanafunzi. Kama mazingira ya Milambo unayajua basi wamekaa kwenye viunga vya majani vilivyopo mbele ya bwalo hilo, na anaenda mmoja mmoja kupiga picha na mkuu wa shule. |
Ukitaka kumfahamu mmiliki wa Maganga Media, (HAYUKO PICHANI) ni sharti uanzie historia yake katika Shule ya Sekondari Milambo iliyoko mkoani Tabora takribani miaka 10 iliyopita alipofika shuleni hapo kwa ajili ya masomo akiwa kama mwanafunzi wa kidato cha kwanza.
Kwa leo sina muda wa kuyakumbuka matukio yote na kuyaweka kwenye hii post, nitajitahidi kuyaweka kadri siku zinavyoendelea. Jambo moja la msingi ambalo sio siri linanikumbusha wajibu wangu kwangu mwenyewe, familia, jamii na Taifa kwa ujumla, ni namna nilivyokabiliana na maisha hayo na mpaka hapa nilipo sasa. Kwa ufupi naweza nikasema ni Mungu tu, kwa akili za kibinadamu haikuwa rahisi.
Tukirudi kwenye picha yetu hapo juu, ni miongoni mwa mahafari ya kidato cha nne mwaka 2003. Tofauti na mahafari zenu siku hizi, (Wanafunzi wa Sekondari) mpaka mshone majoho na vurugu nyingi mji mzima hadi inakuwa kero, harafu matokeo yakitoka mzazi ndio anaanza kujumlisha hasara ya gharama zote alizozipata tangu alipokupeleka shule, na zile zilizoongezeka siku ya mahafari.
Kihistoria tu, hiyo ilikuwa ni mahafari ya kwanza kwa kidato cha nne tangu mkuu wa shule agomee kufanya mahafari yeyote kwa wanafunzi wa O- Level akiwaita ni kizazi cha nyoka, kilichotokana na athari za mgomo wa Oktoba, 2001. Kwa uwezo wa Mungu mwaka uliofuata ilifanyika mahafari nzuri na kubwa iliyogharimikiwa na shule.
Picha kwa hisani ya Mwalimu Masumbuko Ramadhani (Anayepokea cheti katika picha)
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII