HABARI MPYA LEO  

England uso kwa uso na Italy robo fainali!

By Unknown - Jun 20, 2012

Wayne Rooney

Wayne Rooney alikaribishwa kama shujaa katika timu ya England usiku wa Jumanne, baada ya kutokuwepo kwa muda kufuatia adhabu ya UEFA, na bao lake moja dhidi ya Ukraine liliiwezesha timu yake kuwa kileleni katika kundi la D. Vile vile bao hilo linamaanisha England imeweza kuiepuka Uhispania katika robo fainali, na sasa itacheza dhidi ya Italia.

Sweden yaondoka kwa kishindo

Ufaransa na Sweden
Bao lililoingia wavuni kwa ustadi kutoka kwa Zlatan Ibrahimovic limeisaidia Sweden kuishinda Ufaransa magoli 2-0 katika mechi ya kundi D na kuhakikisha wameisukuma Ufaransa katika nafasi ya pili katika kundi, na pia kuilazimisha kukutana na mabingwa watetezi Uhispania katika mechi ya robo fainali ya Euro 2012.

Ufaransa walilemewa katika mechi hiyo, na Ola Toivonen alikaribia kuiletea Sweden bao la kwanza alipogonga sehemu ya nje ya mwamba wa goli. Hatimaye Ibrahimovic alipata bao kupitia mkwaju kutoka yadi 15, baada ya kusukumiwa mpira kutoka kwa Sebastian Larsson. Olivier Giroud alifunga kwa kichwa na kuiwezesha Sweden kupata bao lao la pili.

Kushindwa kwa Ufaransa kuna maanisha hatua yao ya kucheza pasipo kushindwa katika msururu wa mechi 23 zilizopita tangu waliposhindwa wakiwa nyumbani na Belarus mwezi Septemba mwaka 2010 imesitishwa.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII