HABARI MPYA LEO  

YEYE YA LADY JAYDEE YABAMBA MASHABIKI

By Maganga Media - May 14, 2012


MSANII nguli wa bongo fleva nchini Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ ameachia singo yake mpya inayokwenda kwa jina la ‘Yeye’. Msanii huyo mwenye mafanikio ya hali ya juu katika muziki huo ameendelea kuonyesha umahiri alionao katika tasnia hiyo, baada ya kutumia lugha nne tofauti kwenye singi hizo zikiwemo Kiswahili, Kiingereza, Kilingala na Kiganda. 

Jaydee amesema kwamba ameamua kutumia lugha tofauti ili pia kuweza kuwashika mashabiki wa maeneo mengine ambao wamekuwa wakifurahia kazi zake lakini wakitatizwa na lugha. 

Kazi hiyo ambayo imetayarisha katika studio za FishCrab za jijini Dar es Salaam chini ya mtayarishaji Lamar imeshaanza kufanya vema kwenye vituo mbalimbali vya redio na hivyo kuteka nyoyo za mashabiki. Hii ni mara nyingine kwa mwanadada huyo kuachia singo ya yenye lugha tofauti ambapo awali aliwahi kuachia Distance, Mimi ni Mimi alioimba na Oliver Mtukudzi na nyinginezo.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII