HABARI MPYA LEO  

Mfumuko wa bei sasa basi!

By Maganga Media - May 15, 2012

 

WAZIRI wa Fedha, Dk William Mgimwa, amesema tatizo la kupanda kwa gharama za maisha na  mfumuko wa bei unaolitikisa taifa kwa sasa umechangiwa kwa kiasi kikubwa na hatua ya Serikali kuchelewa kupeleka fedha za kununulia nafaka kwa ajili ya kuhifadhi kwenye maghala ya taifa ya hifadhi ya chakula.

Alisema hali hiyo imesababisha kuadimika kwa baadhi ya vyakula sokoni kutokana na usambazaji wake kuwa mdogo ikilinganishwa na mahitaji makubwa yaliyopo nchini jambo ambalo ndilo chanzo kikubwa cha kupanda kwa bei sokoni.

Akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Iringa kuhusu mkakati wa Wizara yake katika kukabilina na mfumuko wa bei, kupaa kwa gharama za maisha,  kuporomoka kwa shilingi ya Tanzania na  kauli tata za wanasiasa wanaodai nchi imefilisika, Dk Mgimwa alitaja baadhi ya vyakula vilivyopanda bei na kiuwatesa wananchi ni pamoja na Mchele, Sukari, Maharage na unga.

Kuhusu hoja za baadhi ya wanasiasa wanaodai kuwa  nchi imefilisika na iko kwenye hali ngumu, Dk Mgimwa alisema kuwa kauli hizo hazina mashiko, kwa madai kuwa nchi ipo salama kutokana na taifa kuwa na  akiba ya Dola3.6 bilioni za kimarekani ambazo zinatosheleza mahitaji ya nchi kwa miezi minne.  

Alifafanua kuwa mpango huo wa kuirejesha shilingi ya Tanzania katika thamani yake, kunatokana na mfumo mpya ulioigwa kutoka katika mataifa ya Italy, Ugiriki, Ireland na Ureno ambazo zimeamua kuondoa fedha zake kutoka katika matumizi ya Euro na kuhamishia akiba yake kwenda kwenye dola.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII