WATANZANIA NCHINI JAPANI WAFANYA MATEMBEZI YA HISANI
By Maganga Media - May 6, 2012
Watanzani wakipeperusha bendera ya Tanzania katika Matembezi ya hisani yaliyoandaliwa na jiji la Yokohama
Mwenyekiti wa watanzania wanaoishi nchini Japani Radhid Njenga (mwenye kanzu) naye alikuwemo.

Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Japani, wamewaongoza watanzania wanaoishi hapa kushiriki katika matembezi ya hisani ya mji wa Yokohama, ikiwa ni moja ya hatua za kukuza urafiki kati ya jiji hilo na Tanzania.
Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania na hata mataifa ya Afrika kushiriki rasmi kwenye matembezi hayo ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka. Mwaka huu, Tanzania kutokana na historia yake ya kupenda, kusimamia na kutetea amani, umoja na mshikamano duniani.
Aidha katika siku za usoni, mji wa Yokohama una mpango wa kuanzisha uhusiano (Sistercity Friendship) na moja ya miji ya Tanzania, uhusiano ambao utajumuisha kupanda miti aina ya Cherry blossom katika mji utakaochaguliwa Tanzania.
Matembezi hayo yalianzishwa mwaka 1953 kwa lengo la kuhamasisha jitihada za kufufua uchumi na utalii wa mji wa Yokohama kufuatia uharibifu uliotokana na Vita Kuu ya Pili ya Dunia.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII