HABARI MPYA LEO  

Chelsea Bingwa FA

By Maganga Media - May 6, 2012


Didier Drogba
Aifungia Chelsea bao la pili na kuiwezesha kupata ushindi katika fainali ya Kombe la FA

Chelsea wamechukua ubingwa wa Kombe la FA Cup kwa mara ya saba, kufuatia magoli kutoka kwa Ramires na Didier Drogba dhidi ya Liverpool. Ramires alifunga kufuatia kosa la Jay Spearing, kabla ya Didier Drogba kufanikiwa kumkwepa Martin Skrtel na kuandikisha bao la pili.

Liverpool walionyesha mchezo duni hadi Andy Carroll alipofunga bao moja baada ya John Terry kukosa kuimarisha ngome ya Chelsea kikamilifu, na mabao kuwa ni magoli 2-1.

Kulikuwa na ubishi kwa muda uwanjani baada ya Carroll kudhani alikuwa amefunga bao la kusawazisha kwa kichwa, na Petr Cech kuutema mpira huo, ambao kwanza uligonga mwamba na kuanguka mbele ya msitari. Wachezaji na mashabiki wa Liverpool wote walidhani mpira ulikuwa umevuka msitari.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII