HABARI MPYA LEO  

WASHINDI TUZO ZA KILL MUSIC AWARDS 2012 WAFUNIKA MWANZA

By Maganga Media - May 7, 2012

Msanii AT kutoka Zanzibar akitumbuiza jukwaani na wacheza sho wake wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba.
Barnaba Boy ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kiume akimbo jukwaani hii leo wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba.
Ben Paul nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta raha kwa mashabiki katika wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba.
Diamond nae alishambulia jukwaa vilivyo na kuleta raha kwa mashabiki katika wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba.
Msanii anae kuja juu Omy Dimpoz nae akikamua jukwaani wakati wa show maalum ya Washindi wa Kili Music Award mkoani Mwanza katika Uwanja wa Kirumba.

Na Ripota  wetu, Mwanza.
WASANII wa Muziki wa Kizazi Kipya Diamond, Roma, Isha Mashauzi, AT, Barnaba, Omy Dimpoz, Ben Paul wamefunika vibaya katika Tamasha la Kili Music Award Winners  Tour lililofanyika katika Uwanja wa Kirumba jijini Mwanza, na kutoa burudani ya uhakika kwa wapenzi wa burudani ya Musiki wa jiji hilo na vitongoji vyake.

Show hiyo kali iliyoanza majira ya saa 8 mchana ikitanguliwa na makundi kadhaa ya wasanii chipukizi wa Bongo Fleva wa Jijini Mwanza ilizidi kupamba moto muda hadi muda hadi pale wasanii Nguli na washindi wa Tuzo za Kili Music Award 2012 walkipowasili uwanjani hapo.

Katika kukuza vipaji na kuibua vipaji vipya vya wasanii chipikizi Msanii Christian Joachim maarufu kama Christian JJ alifanikiwa kuwashinda wenzake wawili akiwepo mwana dada kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Jijini Mwanza Bertha Denis.

Christian JJ aliibuka kidedea baada ya kupata kura nyingi za mayowe zilizo lipuka kutoka kwa mashabiki takribani wote uwanjani hapo na kuungana na mshindi mwingine kutoka mkoani Dodoma ambao wataenda jijini Dar es Salaam kurekodi nyimbo yao moja kwa Mtayarishaji wa Muziki maarufu.

Alianza jukwaani kupanda mwanadada wa Kikurya anaeimba Taarabu, Isha Mashauzi wa Mashauzi Clasic ambaye alijinyakulia Tuzo ya Wimbo bora wa taarabu kupitia wimbo wa Nani kama Mama na kukonga nyoyo za wapenzi wa taarabu vilivyo kwa kuimba vibao vyake kadhaa.

Isha Mashauzi alifuatiwa Jukwaani na mshindi wa Tuzo ya wimbo Bora wa R&B.
Msanii Ben Paul ambaye alijinyakulia tuzo hiyo kupitia kibao Number One ambapo nae alishambulia jukwaa vilivyo.

Omy Dimpoz alifuata jukwaani kwa kuimba nyimbo zake kadhaa ikiwapo ile iliyo mpa tuzo ya Wimbo bora wa Kushirikishwa ya Nai Nain a kusindikizwa na wacheza show wake wanne.

Mshindi wa Tuzo ya Mwimbaji bora wa Kiume, Barnaba alifuata jukwaani na kuimba nyimbo kadhaa na kumpisha Mkali kutoka Zanzibar ambaye ni mshindi wa Tuzo Wimbo Bora wenye Vionjo vya Kiasili AT ambaye aliimba nyimbo kadhaa ikiwepo iliyompa Tuzo ya Vifuu Utundi amabyo aliicheza vilivyo na wanenguaji wake waili wa kike.

Baada ya Kushika AT alipanda tena Barnaba kasha kumpisha Mkali wa Tuzo za Kili Music Award 2012 Diamond ambaye alijizolea Tuzo tatu alipanda jukwaani kwa kishondo huku akiwatanguliza wacheza show wake.

Diamond akishangiliwa vilivyo aliimba sambamba na kucheza nyimbo zake takriban zote huku zilizo mpa tuzo za Wimbo Bora wa Mwaka na ule wa Mawazo uliompa Tuzo bora ya Video bora zikishangiliwa vilivyo.


Diamond ambaye ndiye anazungumzwa kwa sasa kuwa msanii ghali na bora nchini alimudu vyema kushambulia jukwaa na kuwafanya mashabiki muda wote mikono kuwa hewani.

Pazia la Wasanii washindi wa tuzo za Kili Music Award 2012 wanaofabnya ziara na waliobahatika kufika jijini Mwanza lilifungwa na Roma Mkatoliki a.k.a Mpare wa milimani aliyeshambulia jukwaa kwa nyimbo zake kadhaa za mistaari ya maandiko.


Roma ambaye ni Mshindi wa tuzo mbili za Wimbo Bora wa Hip Hop kupitia wimbo wake wa Mathematics na Tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop, alishambulia jukwaa huku viitikio vyake vikiimbwa na DJ Choka.

Wasanii hao wiki ijayo wanataraji kutoa burudani kama hiyo Mkoani Kilimajaro katika mji wa Moshi na tayari walisha tumbuiza na kuwashukuru mashabiki wao wa Mkoani Dodoma kwa kuwapa kura za ushindi.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII