WAKUU WA WILAYA WALIOACHWA
By Maganga Media - May 10, 2012
HATIMAYE Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya zote nchini, huku akiwatupa nje 31 na kuteua wapya 70 kati ya 133 walioteuliwa, ikiwa ni wiki moja tu tangu yafanyike mabadiliko makubwa ya Baraza la Mawaziri.
Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amewahamisha wakuu wa wilaya 48, wakati waliobaki katika vituo vyao vya awali ni 15 tu.
Kabla ya kutangazwa jana, nafasi za wakuu wa wilaya 20 zilikuwa wazi kutoka na sababu mbalimbali, zikiwamo waliokuwa wakuu wake kuteuliwa kushika nafasi nyingine za uongozi ndani na nje ya Serikali.
Katika mabadiliko hayo, Rais Kikwete amewahamisha wakuu wa wilaya 48, wakati waliobaki katika vituo vyao vya awali ni 15 tu.
Kabla ya kutangazwa jana, nafasi za wakuu wa wilaya 20 zilikuwa wazi kutoka na sababu mbalimbali, zikiwamo waliokuwa wakuu wake kuteuliwa kushika nafasi nyingine za uongozi ndani na nje ya Serikali.
Walioachwa
Uchambuzi zaidi umebaini kuwa miongoni mwa walioachwa na wilaya zao kwenye mabano ni pamoja na Evans Balama (Mbeya), Zainab Kukwega (Makete), Samwel Kamote (Bukoba), Salum Nyakonji (Ngara) na Othman Mdoe (Mwanga).
Wengine walioachwa ni Musa Samizi (Moshi), Hawa Mchopa (Ruangwa),Dk Ian Lengibori (Babati), Winfrid Ligubi (Hanang), Frank Uhaula (Kiteto), Geofrey Ngatuni (Musoma Mjini), Esther Wakali (Ileje), Gabriel Kimoro (Mbozi) na Kanali John Mzurikwao (Sumbwanga).
Wengine walioachwa ni Joyce Mgana (Nkansi), Philimon Shelutete (Geita), Zainabu Kondo (Magu), Henry Clemence (Mkuranga), Thomas Ole Sabaya (Songea), Kanali Edmund Mjengwa (Mbinga), Bahati Matala (Kahama) na Grace Mesaki (Iramba).
Pia wamo Florence Horombe (Nzega), Stanley Kolimba (Uyui), Kapteni Seif Mpembenwe (Handeni) na Rashid Ndaile (Mkinga).
Kwa upande wa nafasi 20 ambazo zilikuwa wazi, uchambuzi wetu umebaini kuwa zilitokana na wakuu wa wilaya tatu kuchaguliwa kuwa wabunge ambao ni Naibu Waziri wa Nchi (Tamisemi – Elimu) Kassim Majaliwa, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba na mtangulizi wake kabla ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, Athumani Mfutakamba ambaye pia ni mbunge wa Igalula.
Kwa upande wa wakuu wa wilaya 15 waliopandishwa vyeo kwa kuteuliwa kuwa wakuu wa mikoa ambayo iko kwenye mabano ni John Tupa (Mara), Saidi Mwambungu (Ruvuma), Chiku Gallawa (Tanga), Leonidas Gama (Kilimanjaro), Dk. Rehema Nchimbi (Dodoma), Elaston Mbwillo (Manyara) na Kanali Fabian Massawe (Kagera).
Wengine ni Fatma Mwassa (Tabora),
Ali Rufunga (Shinyanga), Ernest Ndikillo (Mwanza), Magesa Mulongo (Arusha), Dk Rajab Rutengwe (Katavi), Magalula Saidi Magalula (Geita), Paschal Mabiti (Simiyu) na Kapteni Asery Msengi (Njombe).
Nafasi nyingine mbili zilibaki wazi baada ya Nape Nnauye kuteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM wakati aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Cleophace Rugarabamu nafasi yake ilibaki wazi baada ya kufariki dunia.
Walioteuliwa
Waandishi wa habari ambao wameteuliwa kuwa wakuu wa wilaya ni pamoja na aliyekuwa Naibu Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Jacqueline Liana na aliyewahi kuwa Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Ltd, Muhingo Rweyemamu.
Wengine ni Mtangazaji wa zamani wa iliyokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Ahmed Kipozi, Mtangazaji wa kituo cha Televisheni cha ITV mkoani Arusha, Novatus Makunga na Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji (TBC), Suleiman Mzee.
Kwa upande wa wabunge wa zamani wamo Ponsiano Nyami, Suleiman Kumchaya, Dk Charles Mlingwa, Manju Msambya, Omar Kwaangw’, Venance Mwamoto, Benson Mpesya, Daudi Felix Ntibenda, Ramadhani Maneno, Gulamhusein Kifu na Esterina Kilasi.
Kadhalika yumo aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Amani Mwenegoha na wabunge wa viti maalum ambao ni Martha Umbula, Rosemary Kirigini na Lucy Mayenga.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII