HABARI MPYA LEO  

Picha ya mlipuko wa bomu Nairobi!

By Maganga Media - May 29, 2012

Inaaminika kwamba ni idadi kubwa ya watu waliopelekwa hospitali kutokana na kujeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu Nairobi Kenya leo Moi Avenue street, ulipuaji huo wa bomu unaaminika kufanywa na kikundi cha wanamgambo wa Al Shabaab Somalia.
Jengo la pili kutoka kulia ndio lililolipuliwa, Kwa mujibu wa Nation.co.ke ni watu 30 waliojeruhiwa, polisi walikanusha kwamba sio bumu ni shoti ya umeme la shirika la umeme Kenya limekanusha kwa kusema sio shoti manake hakuna transfoma kwenye eneo la tukio ila ingekuepo ndio kungekua na uwezekano wa shoti.
Mlipuko huo ulifanya baadhi ya majengo mengine ya karibu kutingishika ambapo ulitokea kwenye saa saba na dakika kumi leo mchana, mpaka sasa haiko wazi ni wangapi wamejeruhiwa au kupoteza maisha.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII