HABARI MPYA LEO  

Maonyesho ya wanafunzi wa UDOM katika ukumbi wa Chimwaga

By Maganga Media - May 28, 2012

 Muandaaji wa Maonyesho haya Ester Zangi ambaye pia ni Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 anayesomea shahada ya kwanza ya sayansi ya siasa na utawala wa umma(Wa Kwanza Kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ambao Wameonyesha vipaji vyao Vya Kuchora Michoro inayoonekana hapo katika maonyesho yaliyofanyika leo Chuo Kikuu Cha Dodoma katika Ukumbi wa Chimwaga
 Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 anayesoma shahada ya kwanza ya filamu na sanaa anayejulikana kwa jina la wacko jack akiwa amesimama pembeni mwa moja ya michoro aliyochora kwa Mikono yake na hapo alikua katika maonyesho yaliyofanyika chuo kikuu cha Dodoma leo
Mmiliki na Mwendeshaji wa Mtandao wa Lukaza Blog Mh Josephat Lukaza alipokua akitoa maelekezo jinsi ya Lukaza Blog inavyofanya kazi na vilevile Mtandao wa Lukaza Blog unavyopatikana na ulivyoweza kupokelewa Vizuri Katika Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakati wa Maonyesho yaliyofanyika Chuoni hapo leo
Mmoja wa wanakamati wa maandilizi ya maonyesho haya ambaye pia ni mwanafunzi wa mwaka wa 3 Bi Atu anayesoma shahada ya kwanza ya Mazingira ya Chuo Kikuu Cha Dodoma alipokua akitoa neno wakati wa maonyesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) leo
Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 kutoka kitivo cha mawasiliano na kompyuta Mwinula Peter Kingamkono alipokua akionyesha na kutoa maelezo juu ya Mtandao wa Kijamii Wa Michezo ya Mtandaoni(Game Social Network) unavyofanya kazi katika maonyesho yaliyofanyika katika Ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) leo
Muonekano wa Mtandao wa Kijamii Wa Michezo ya Mtandaoni (Game Social Network) ambao Mwanzilishi wake pichani alipokua akiutolea ufafanuzi jinsi unavyofanya kazi
Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Ambaye pia ni Mwanafunzi wa Shahaada ya kwanza ya Utalii ya Chuo Kikuu Cha Dodoma alipokua akitoa Burudani wakati wa maonyesho ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuoni hapa
Wanafunzi wa UDOM wanaosoma shahada ya kwanza ya Filamu na Sanaa, Kiswahili wakionyesha uwezo wao wa kucheza boringo katika tamasaha lililofanyika leo Katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Cah Dodoma (UDOM)
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma waliohudhuria maonyesho hayo leo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)
Mmoja wa Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sanaa na Filamu Babra Kalugira akiwa kwenye Kirekodi Video (VIDEO CAMERA) akichukua video ya matukio yaliyokuwa yakiendelea katika Maonyesho hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Chimwaga uliopo Chuoni Hapo

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII