HABARI MPYA LEO  

Kanumba kuenziwa ulaya

By Maganga Media - May 14, 2012


MSANII Steven Kanumba anaendelea kuenziwa kwani huko barani ulaya Watanzania ambao hawakupata nafasi ya kuja nchini kushiriki mazishi, wameandaa tamasha la kumuenzi gwiji huyo wa filamu aliyefariki mwezi uliopita.

Mtandao wa www.filamucentral.co.tz unaandika kuwa tamasha hilo litawakusanya wapenzi wa Kanumba kutoka Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, na Uholanzi alisema mmoja wa watayarishaji.

“Tumeguswa sana na kifo cha Kanumba, tulipenda kuja kushiriki mazishi yake lakini ilikuwa ni ghafla na kulikuwa na haraka kuzika, kwa hiyo tulitaka kufanya tamasha la kumuenzi huku kwa sababu tulihitaji wasanii aliofanya nao kazi waje huku, tunahitaji kuwasiliana nao kwa sasa,”anasema Chansad Mundele.

Jami Burundi wanaoandaa tamasha hilo wamesema wanatarajia kulifanya mwezi ujao.Wasanii wengi kutoka Bongo watashiriki katika tamasha hilo.
 

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII