HABARI MPYA LEO  

Facebook inauza hisa zake

By Maganga Media - May 19, 2012

Wafanyakazi wa kampuni ya Facebook


Mtandao wa kijamii wa Facebook utaanza kuuza hisa zake baadaye kwenye soko la hisa la New York, katika mkupuo mkubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa wa uuzaji wa hisa katika miaka ya hivi karibuni. Mwasisi wa mtandao huo, Mark Zuckerberg alifungua biashara katika soko la hisa la Nasdaq ingawa hisa za Facebook hazitauzwa hadi baadaye.

Hisa za kampuni hizo ziligonga thamani ya zaidi ya dola bilioni moja. Mkupuo wa kwanza uliotolewa, ambao ni mkubwa kuwahi kutolewa, uliingiza zaidi ya dola bilioni 18 kwa mtandao wa Facebook na wanahisa wake waliopo katika biashara.

Tangu kuanzishwa kwake, miaka nane iliyopita, Facebook ni moja ya kampuni zenye teknolojia ya thamani ya hali ya juu miongoni mw kampuni za mitandao ya kijamii. Kampuni hiyo ina watumiaji wa kila mara wa huduma zake wapatao milioni mia tisa.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII