HABARI MPYA LEO  

Chelsea kazi nzito!

By Maganga Media - May 19, 2012


Chelsea
Wachezaji wa Chelsea wana kibarua kigumu
Hatimaye Chelsea wanaingia uwanjani leo katika hatua ya mwisho ya jitihada zao za kutwaa Kombe la Mabingwa Ulaya. Chini ya kocha wa muda, Roberto Di Matteo, Chelsea wana kazi ngumu bado, kwani watakuwa Allinz Arena, nyumbani kwa Bayern Munich, wakikabiliana nao kwenye fainali.

Kama ndoto vile, katika nusu fainali, Chelsea iliwashangaza wengi, kwa kuisambaratisha timu bora Ulaya na duniani, Barcelona. Fainali ya wikendi hii ni wazi itakuwa ngumu kwa timu zote, huku Chelsea wakiwa wameshajijenga kisaikolojia na kujiamini kwamba wanaweza.

Hata kocha wa Bayern Munich, Jupp Heynckes anaamini kwamba, kwa timu yake kucheza nyumbani, ina nafasi kidogo tu juu ya Chelsea, anaosema ni hatari.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII