HABARI MPYA LEO  

Beckham apunguziwa Mshahara!

By Maganga Media - May 28, 2012

David Beckham



MWANASOKA nyota, David Beckham amepunguziwa mshahara kwa zaidi ya dola za Kimarekani Milioni mbili — ambayo ni sawa na kushuka kwa asilimia 40 ya pato lake.

Inamaanisha nyota huyo wa LA Galaxy ameondoka kwenye orodha ya wanasoka wanaolipwa fedha nyingi katika Ligi ya Marekani, akina Thierry Henry, ambaye anachezea New York Red Bulls.
Becks, mwenye umri wa miaka 37, amekuwa akilipwa zaidi ya pauni Milioni 4 (dola Milioni 6.5) kwa mwaka.
Lakini amekubali kulipwa pauni Milioni 2.5, baada ya kuamua kubaki California na mkewe Victoria, mwenye umri wa miaka 38, na watoto wao wanne.
Pamoja na hayo, anapata makato ya mauzo ya tiketi za Galaxy na vifaa vya michezo. Na ataendelea kupata kiasi cha jumla ya pauni Milioni 29 kwa mwaka, kupitia dili za mauzo ya nguo  na maslahi ya kibiashara, ( jarida la Forbes.)
Nahodha huyo wa zamani wa England, Becks angeweza kujiingizia fedha nyingi zaidi kama angekubali kuhamia Paris Saint-Germain.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII