Arsenal 3 Norwich 3
By Maganga Media - May 5, 2012
Grant Holt aliiwezesha Norwich kufunga bao la pili na kuipatia timu hiyo matumaini ya kupata ushindi, lakini Robin van Persie akatandika mkwaju ambao kipa kabisa hakuwa na nafasi ya kuupata mpira.Bao la Morison katika dakika za mwishomwisho ziliwawezesha kuondoka na pointi moja.
Matokeo hayo yanamaanisha Arsenal imecheza mechi nne za mwisho pasipo kupata ushindi, na kuipunguzia matumaini ya kumaliza ligi katika nafasi ya nne bora kuiwezesha kushiriki katika mechi za klabu bingwa barani Ulaya.
Hatma ya Arsene Wenger na vijana wake wa Gunners, na ambao wamo katika nafasi ya tatu, huenda ikabadilika kufuatia matokeo ya mechi za Jumapili, wakati wapinzani wao wa kaskazini mwa London, Tottenham, watakaposafiri kucheza na Aston Villa, huku Newcastle nao wakiikaribisha Manchester City.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII