HABARI MPYA LEO  

Some Indonesians opposed Lady Gaga's scheduled performance, accusing her of being a 'devil worshipper' [EPA]. Cancellation of US pop star's Jakarta concert raises fears that hardliners may be pushing an agenda of intolerance. "Little monsters lost to big monsters", wrote an Indonesian television anchor on his Twitter account shortly after Lady Gaga cancelled her biggest concert in Asia, a sold-out event scheduled to take place in Jakarta on June 3.

The pop star's fans, which she affectionately calls her "little monsters", now have to accept that the woman they saw on Indonesian television, or discovered in DVD shops, cannot visit their country because of safety concerns. Although a small group of Islamic hardliners rejoiced over the news of Gaga's concert cancellation, many Indonesians started to wonder who really has gone gaga here.

In fact, this incident does not have much to do with the American singer. Instead, it illustrates a far deeper conflict that is dividing Indonesia. The Lady Gaga saga started a few weeks ago, after some Indonesians opposed her visit, citing her exposed body parts and "devilish" lyrics.

The pop star soon became the centre of a debate between those who see her as a symbol of freedom, and those who see her as a symbol of evil. The fact that the Islamic Defenders Front (IDF) was successful in repelling her from Indonesia shows that threats of violence can pay off. "The fact that police can't guarantee security of the concert shows that our state is weak towards groups that promote intolerance," said Hendardi, head of the Setara Institute for Democracy and Peace.

"It's up to the authority of the state to guarantee freedom of expression and security as outlined in our constitution."


As people share more and more of their lives via social media, The Stream speaks to Andrew Keen, who says the online social revolution is dividing and diminishing us. He argues that Facebook is making people narcissistic. Keen’s unapologetic support for copyright and intellectual property rights has garnered criticism from those who believe such laws inhibit online sharing.

While fans of social media argue it connects people all over the world, Mr. Keen counters it actually pulls people farther apart and reduces their humanity. 

The social media boom has grown over the last decade to include millions around the world. It's become a major industry, with Facebook's IPO being one of the biggest in years. So is social media here to stay, or could something replace it? This video argues that it's going to become an even bigger part of every day life.

Andrew Keen is a critic of social media. In his latest book, #digitalvertigo, he warns about the dangers posed by over-sharing on social media: namely, a lack of privacy, increased narcissism, companies exploiting users' data for profit and a growing isolation among members of society.

SPEAK OUT TO SHARE YOUR EXPERIENCE WITH OTHER PEOPLE. COMMENT ON THIS POST !
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla  akikabidhi kiasi cha shilingi milioni kumi kwa mama wa marehemu Steven Kanumba ikiwa ni rambirambi ya Serikali kwa familia.
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi bendera kwa Timu ya Taifa ya mchezo wa Golf inayotarajiwa kusafiri kwenda Gaborone Botwsana kwa ajili ya mashindano ya chalenji ya Afrika kwa upande wa Wanawake.Wapili kushoto ni Mh. Mery Chatanda (Mbunge).
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akikabidhi bendera kwa Kapteni wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu Juma Kaseja,timu hiyo inatarajiwa kusafiri leo kwenda Ivory Coast kwa ajili yakuwania tiketi ya kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.


 Baadhi ya warembo wanaowania taji la Miss Dar Inter College 2012 wakiwa katika pozi mara baada ya mazoezi yao ya kila siku yanayofanyika kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa warembo hao Marylydia Boniface akiwapa maneno mawili matatu warembo hao.



NAibu waziri wa habari, vijana, Utamaduni na Michezo Amos makalla akimkabidhi bendera ya Taifa Nahodha wa Stars Juma Kaseja, wakati wa hafka ya kuiaga timu hiyo leo kwenye hoteli ya Tansoma.Stars inaondoka alfajir ya kesho kwenda Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wao wa mchujo wa komve la Dunia utakaopigwa juni mbil.Wengine ni meneja wa bia ya Kilimanjaro inayoidhamini9 timu hiyo George Kavise, Mwenyekiti wa BMT Dioniz Malinzi na Kocha wa Stars, Kim Poulsen.

KOCHA mkuu wa timu ya Taifa Taifa Stars amewataka wachezaji wake kutohofia nyota waliopo katika kikosi cha  Ivory Coast  kwani hawana tofouti na wao. Stars na Ivory Coast watachuana  Juni 2, mjini Abidjan, katika mechi ya kuwania kucheza fainali za kombe la dunia ambapo kikosi cha Ivory Coast kinawachezaji wanaosakata soka la kulipwa barani Ulaya wakiwemo  Didier Drogba, . Yaya Toure na Solomon Kalou na wengineo.
 
Kim alisema wanaiheshimu Ivory Coast kama moja ya timu yenye wachezaji wazuri lakini hawaihofii kwani wachezaji wa Stars pia ni wazuri ingawa wanatofaitiana vitu vidogo vidogo tu.
 
Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kupambana kadiri wawezavyo katika mchezo huo kwani  ndio siri ya ushindi na mafanikio ya timu yoyote.


 Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili (pichani) akizungumzia uchaguzi huo ambapo amewataka wanachama wote ambao hawajalipa ada kufanya hivyo ili kuweza kushiriki katika mkutano huo. 
Alisema kupitia uchaguzi huo zitajazwa nafasi za Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne ambapo wanachama wayakaowania uongozi wanatakiwa kuwasilisha fomu zao wakiambatanisha risiti ya kununulia fomu, vyeti vya shule, uthibitisho wa uraia, namba ya uanachama na picha mbili za passport size.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakitembea kwa miguu kuelekea kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea  kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiangalia shamba la kahawa wakati wakielekea  kwenye sehemu waliyotengewa kufanyia mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakiwa katika mazungumzo rasmi katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais  Allasane Ouattara  wa Ivory Coast wakipiga picha ya pamoja katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha leo May 30, 2012 ambako Rais huyo wa Ivory Coast amefika kuhudhuria mkutano wa afDB ambao unbafunguliwa rasmi kesho na Rais Kikwete katika ukumbi wa AICC. Katika maongezi yao Rais Kikwete amesema Tanzania inaunga mkono juhudi za Ivory Coast za kutaka kurejesha nchini humo makao makuu ya afDB ambayo yamehamia Tunisia kutokana na vurugu zilizotokea Abidjan baada ya uchaguzi mkuu mwaka jana.
Mwigizaji Wema Sepetu bado anaendelea kuishoot movie yake ya kwanza iitwayo SUPER STAR ambayo inahusiana na maisha yake kwa asilimia kubwa sana, ikiwa ni movie ambayo itaonyesha vitu vingi alivyovipitia kwenye umaarufu wake.
 Wema Sepeta na Bodyguard wake
Usiku wa May 29 kuamkia may 30 2012 saa nane na dakika kumi ndani ya Maisha Club Dar es salaam, Wema alivishwa pete na mwimbaji Mwinyi wa Machozi Band ambae kwenye hiyo movie yeye atazicheza nafasi zote za Mwimbaji Diamond Platnums aliyewahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Wema Sepetu, Mwinyi amecheza kama Diamond ambae pia alimvisha Wema pete ya uchumba hapohapo Maisha Club.
 Wema & Abou
Wema amesema bajeti ya kutengeneza hiyo movie ni kuanzia milioni 29 mpaka 30 ambapo alianza kuitengeneza machi mwaka huu na ataizinduaJune 23 2012.
Mrembo huyu ambae ni Miss Tanzania 2006 amesema mwanzoni alikua anataka hii movie wacheze Irene Uwoya na Jb na ilikua haikua ikihusu maisha ya Wema lakini baada ya Jb kuwa na kazi nyingi, alifikiria kucheza movie mwenyewe na kupewa idea ya Super Star na msanii Suma Lee. Alichofanya baada ya kupewa hiyo idea na Suma Lee ni kuipimp na kuongeza matukio mengi aliyokutana nayo kwenye umaarufu na ni movie ambayo mastaa wengi wa kibongo wameuza sura ndani yake.

Mario Balotelli nyota wa soka nchini Italia ambaye pia ni mchezaji mweusi wa Klabu ya Manchester City ya Uingereza amesema ataondoka uwanjani endapo atakejeliwa kutokana na rangi yake wakati wa mchuano wa kombe la Mataifa Ulaya katika nchi za Poland na Ukraine mwezi Juni. Matamshi yake yanatokea kufuatia makala ya BBC ambayo yaliangazia ghasia katika viwanja vya soka kutokana na ubaguzi wa rangi katika nchi hizo mbili.

Makala hayo yalionyesha mashabiki wakizungu wakiwakejeli wachezaji weusi na kuwashambulia mashabiki wenye asilia tofauti na kizungu.

Wanasiasa na maafisa wa soka kutoka nchi hizo wamesema tatizo hilo limetiwa chumvi. Kukejeliwa kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya Balotelli nchini Italia mwaka 2009 kulifanya shirika la soka Ulaya UEFA kuweka sheria ya kuwalazimisha marefa kusimamisha mechi ikiwa kejeli za ubaguzi wa rangi zitaendelea.

Rais wa zamani nchini Liberia Charles Taylor amehukumiwa miaka 50 jela na makahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita. Mwezi jana Taylor alipatikana na makosa ya kuwaunga mkono waasi nchini Sierra Leone katika vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 1991 na 2002.
Upande wa mashtaka ulitaka kiongozi huyo wa zamani kusukumwa jela miaka 80. Charles Taylor amesisitiza hana hatia yeyote na anatarajiwa kukata rufaa. Akitoa hukumu hiyo Jaji Richard Lussick amesema dhuluma zilizotekelezwa nchini Siera Leone zilikuwa za kinyama zaidi kuwahi kushuhudiwa katika historia ya binadamu. Mahakama maalum ya Kimataifa inayochunguza dhuluma za kivita nchini Sierra Leone ilimpata Taylor na hatia ya makosa 11 dhidi ya binadamu ikiwemo mauaji na ubakaji.

Taylor amekuwa Rais wa kwanza kuhukumiwa kwa makosa ya vita na Mahakama ya Kimataifa tangu kesi za Nuremurgs dhidi ya watawala wa Kinazi baada ya Vita Kuu ya Pili duniani. Kesi dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Liberia inasikilizwa The Hague kwa hofu kwamba kufanyika kwake Sierra Leone huenda kukazua vurugu katika kanda hiyo. Taylor anatarajiwa kuhudimia kifungo chake nchini Uingereza.
Wema sepetu mweeee!!!! Aweka historia kwa mara nyingine tena leo Wema Sepetu kuvishwa pete na Mwinyi wa Machozi Band ndani ya NEW MAISHA CLUB usiku wa kuamkia leo
 Mtu mzima Mwinyi akaenda chini pwaaaa...

 Akakumbatiwa watu weweeeeeee


 Heeeh si akaweka pete kidoleni pale kabaaaaaaa

 Mabusu hihaaaaa, watu pipooooo




 Wema Sepeta na Bodyguard wake


 Wema & Abou


 mmmmh....




Shirika la kuteteta maslahi ya watoto la The African Child Policy Forum linasema zaidi ya watoto elfu 40 wameasiliwa katika kipindi cha miaka minane wengi wakiwa na walezi kutoka Marekani, Ulaya Magharibi na Canada. Watoto wengi hasa wanaasiliwa kutoka Ethiopia ambayo inatuma watoto wengi ugenini nyuma ya China.
 
Kuna zaidi ya mashirika 70 yanayoshughulika na mpango wa kuwaasili watoto nchini Ethiopia 15 ya mashirika yakiwa ni ya Kimarekani.

Sababu kubwa ya barani Afrika kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaoasiliwa na wageni ni kutokana na udhibiti mkubwa wa mpango huu katika mataifa ya Ulaya na Amerika Kusini.
The African Child Policy Forum inasisitiza haja ya kila mtoto kukulia katika mazingira yake asilia ya kuzaliwa. Shirika hili linasema ni muhimu kwa mtoto kukua na jamaa na utamaduni anaofahamu zaidi.

NI KUJIBU MASHTAKA YA UFISADI UDA, AJIDHAMINI KWA MALI YA SH8 BILIONI BADALA YA SH500 MILIONI ILIYOTAKIWA  
 
MWENYEKITI wa Bodi ya Shirika la Usafiri  Dar es Salaam (Uda) Ltd, Iddi Simba, jana alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manane, likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka na kulisababishia shirika hilo hasara ya Sh2.4 bilioni.Mbali na Simba ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, washtakiwa wengine ni Meneja Mkuu wa Uda, Victor Milanzi na Mkurugenzi wake Salim Mwaking’inda ambaye pia aliwahi kuwa Diwani wa Kata ya Sinza (CCM).

Baada ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Benny Lincoln kumaliza kuwasomea mashtaka yanayowakabili, aliieleza mahakama hiyo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umeshakamilika na wanaomba kesi ipangiwe tarehe ya kutajwa kabla ya kupangiwa  tarehe ya maelezo ya awali. Wakili Said El- Maamry anayemtetea Simba na mwenzake, Alex Mgongolwa waliiomba Mahakama impatie dhamana mteja wao hoja ambayo haikuwa na pingamizi kutoka kwa Lincoln ambaye alisema mashtaka yanayowakabili washtakiwa yanadhaminika.

Ili kujidhamini, Hakimu Mfawidhi, Ilvin Mgeta aliwataka washtakiwa kutoa hati ya nyumba na kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, kila mmoja wao asaini bondi ya Sh500 milioni.

Baada ya kutolewa kwa masharti hayo, Simba aliwasilisha hati ya nyumba yenye thamani ya Sh8 bilioni na kuridhia wenzake waitumie kupata dhamana.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa hati hiyo ya nyumba ni ya kiwanda cha Kays Hygiene Products Ltd, kilichoko Mikocheni eneo la Viwanda, Plot namba 23, kinachomilikiwa na Simba na mkewe Khadija.

Simba ni Mwenyekiti wa Taasisi ya mikopo kwa Wajasiriamali ya Pride (T) Ltd na Mwenyekiti wa Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam. Akisoma hati ya mashtaka jana Lincoln alidai kuwa  Septemba 2, 2009 Dar es Salaam, Simba na Milanzi  walikula njama ya kuchepusha fedha kinyume na Kifungu cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 11 ya 2007.

Lincoln alidai kuwa Simba na Milanzi walighushi barua  wakionyesha kuwapo kwa kiwango zaidi cha fedha kwenye akaunti zote za benki za Uda wakati wakijua kuwa si kweli. Aliongeza kuwa siku hiyo hiyo, Simba na Milanzi kwa pamoja, walichepusha Sh320 milioni wakijifanya ni malipo ya awali ya mauzo ya hisa katika shirika hilo fedha ambazo walijipatia kutokana na nyadhifa zao.

Washtakiwa hao wote kwa pamoja wanadaiwa kuwa  kati ya Septemba 9 na Februari 11, 2011 wakitekeleza majukumu yao, kwa makusudi walitumia vibaya madaraka yao kwa kugawanya hisa 7,880,330  zisizotumika za UDA kitendo ambacho ni uvunjwaji wa masharti ya vifungu vya ushirikiano katika kampuni  na Kifungu cha 74 cha Sheria ya Makampuni Sura ya 212 iliyorekebishwa mwaka 2002.

Mwendesha mashtaka huyo wa Takukuru, alidai kuwa Februari 11, 2011 washtakiwa hao walishindwa kuchukua tahadhari zinazostahili, walimuuzia Simon hisa milioni 7,880,303 zisizotumika za Uda kwa bei ya Sh1,142,643,935  bila kufuata utaratibu wa zabuni ambao ungeweza kutoa nafasi kwa mnunuzi kutoa ofa ya bei inayolingana na thamani ya hisa hizo, jambo ambalo liliisababishia Uda hasara ya Sh2,378,858,878.80.

Petr Cech
Petr Cech ameamua atasalia katika klabu ya Chelsea, angalau kwa miaka mine ijayo, kufuatia kutia saini mkataba wa muda huo.  Kipa huyo ambaye amehudumu Chelsea kwa muda mrefu, ameichezea timu ya The Blues katika mechi 369, tangu alipojiunga na klabu mwaka 2004.Ataichezea Chelsea kwa miaka minne ijayo. Sasa atakuwa Stamford Bridge hadi mwaka 2016.

"Ninafurahi mno kuwa ni sehemu ya klabu hii maarufu kwa kipindi cha miaka mine zaidi," alielezea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. "Ninatumaini miaka hiyo minne ijayo itakuwa ni sawa na miaka minane ambayo nimekuwa nikikichezea klabu."

Cech, ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa umalizike mwaka ujao, ni mchezaji muhimu kwa Chelsea
Baadhi ya mafanikio ya Chelsea Cech akiwa ni kipa ni pamoja na kupata ubingwa wa ligi kuu ya Premier mara tatu, ubingwa wa Kombe la FA mara nne, ushindi wa Kombe la Carling mara mbili, na hivi majuzi, ubingwa wa UEFA wa klabu bingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza.

Cech pia alitangazwa kama mchezaji bora zaidi wa Chelsea mwaka jana, 2010/11.
MTOTO mmoja amezaliwa jijini Karachi nchini Pakistan akiwa na miguu sita na amefanyiwa upasuaji kuondoa iliyozidi.

Elvan Stambuli na Mitandao


Jopo la madaktari waliomfanyia upasuaji huo Alhamisili iliyopita kwenye taasisi iitwayo National Institute of Child Heath (NICH), jijini Karachi wamesema upasuaji ulikwenda vizuri kama walivyopanga.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Dk. Jamal Raza ambaye pia ni mkurugenzi mkuu wa NICH, alisema miguu mingine iliondolewa kwa operesheni na hali hiyo hutokea mara chache sana.


“Kati ya watoto milioni moja, anaweza kutokea mmoja tu kukumbwa na hali hiyo kutokana na maradhi ambayo kitaalamu huitwa Genetic Disease. Mtoto huwa si wa kawaida,” alifafanua Dk. Raza. 


Alisema mtoto huyo kabla hajafanyiwa upasuaji alipimwa na kipimo maalum, CT Scan ndipo walipoamua kumfanyia upasuaji uliochukua saa nane.


Baba wa mtoto huyo ambaye hajapewa jina, Imran Shaikh, alisema ameshukuru mtoto wake kupata tiba hiyo na sasa amekuwa kama watoto wengine. “Sisi ni maskini, naishukuru serikali kwa kusaidia tiba ya mwanangu,” aliwaambia wanahabari.
Kanisa katoliki lililochomwa moto juzi Mpendae Zanzibar
TAMKO LA ASKOFU MKUU WA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD, DK.BARNABAS MTOKAMBALI, KUHUSU MATUKIO YANAYOASHIRIA UVUNJIFU WA AMANI  NCHINI.

Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na mfululizo wa matukio yanayoashiria
uvunjifu wa amani, umoja na utengamano wa taifa letu la Tanzania, haya
ndiyo yanayonisukuma kutoa tamko hili leo ili kuonya na kushauri.

Katika siku za karibu kiumeibuka makundi mbalimbali ya kidini ambayo
yalianza kutoa matamko yenye kuchochea ghasia za kidini Tanzania, na
pengine kauli hizo ndizo zinazotimizwa kwa vitendo hivi sasa.

Miongoni mwa matukio hayo ni:
Januari sita mwaka huu, kikundi kimoja kinachoitwa JUAKATA, kiliitisha
kongamano la kujadili katiba mpya Tanzania, kwa upande wa Waislam.
Katika kongamano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,
Dar es Salaam kauli zifuatazo:
1. Lazima Rais ajaye atoke Zanzibar
2. Kukabiliana na ukuaji wa kasi wa dini ya Kikristo
3. Kupinga Muungano ili kuupa nguvu Uislamu
4. Kupigana kufa na kupona kutetea maslahi yao wakati huu wa kuandaa
katiba mpya.

Kauli hizo zilitolewa na Sheikh Nasor Mohameed, kutoka Zanzibar,
ambaye alikuwa mgeni rasmi. Baadaye zikaandaliwa kanda za CD
zilizosambaza ujumbe huo.

Uchunguzi unaonesha kuwa miongoni mwa makanisa yaliyochomwa hivi
karibuni huko Zanzibar ni ya EAGT, Elimu Pentecost na TAG, Anglikana,
Katoliki na FPCT, hivyo kujenga taswira ya ubaguzi wa kidini ambao
kama hautapatiwa dawa unaweza kuligawa taifa la Tanzania kama
ilivyotokea Nigeria na kwingineko barani Afrika.

Hofu yangu ni kuwa, roho hii ya ubaguzi wa kidini ambayo Baba wa Taifa
hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliifananisha na dhambi ya kula
nyama ya mtu, imekuwa ikiyatafuna mataifa ya Afrika kama ifuatavyo:

1. Mwaka 2000, vuguvugu la kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu
(Sharia), lilianza kwenye majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria, miaka
michache baadaye majimbo kadhaa yakajitangazia sheria hizo na tangu
wakati huo kumekuwa na mapambano yasiyoisha. Takwimu zinaonesha kuwa
katika miaka ya karibuni zaidi ya Wakristo 500 wameuawa kikatili na
makanisa kuchomwa moto.

2. Roho hii imekuwa ikienea kwa kasi katika maeneo mbali mbali ya
Afrika ambapo imelikumba taifa la Mali, majimbo ya kaskazini tayari
yametangaza kujitenga na kuna vuguvugu lenye kuhusisha mapigano ya
silaha.

3. Itakumbukwa kuwa wiki chache tu zilizopita vuguvugu hili la kudai
utawala wa kidini liliibuka nchini Kenya ambapo watu wanaojiita
wanaharakati walianzisha madai ya kutaka eneo la Pwani kujitenga na
Jamhuri ya Kenya na kujitangazia taifa la Kiislamu.

4. Ni wakati huu ambao kundi la Uamsho linalopinga kuandikwa kwa
katiba mpya kabla ya kuitishwa kwa kura ya maoni ili wanzazibar waamue
kuhusu Muungano liliibuka na kuanzisha ghasia Zanzibar ambazo
zimepelekea makanisa kadhaa kuchomwa moto na mali kuharibiwa, huku
watu wa bara wakitishiwa maisha.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI NA VIONGOZI WA DINI

Ni wajibu wa kila Mtanzania kutii sheria na mamlaka kwa kuwa zimewekwa/
kuruhusiwa na Mungu, hivyo kuziasi ni Kumuasi Mungu, yaani ni dhambi.
Hivyo kila Mtanzania anastahili kukumbuka wajibu wake wa kutii
mamlaka.

Viongozi wenzangu wa dini wakumbuke kuwa wana wajibu mkubwa katika
jamii, na jamii inawasikiliza hivyo ni vyema wakawa makini katika
matamshi na maelekezo yao ili wasiwe chanzo cha kuchochea vurugu za
kidini na uvunjaji wa amani.

Ni vyema wakati huu wa kuandikwa kwa katiba mpya, kila kikundi
kikafuata utaratibu uliowekwa badala ya kuchochea ghasia ambazo
madhara yake yatawakumba watanzania wote ikiwa ni pamoja na wao
wenyewe watoto na wajukuu zao.

Pia ningependa kuwashauri viongozi wa serikali kusimama imara katika
kusimamia sheria na haki, na kuepuka kauli au vitendo vitakavyofanya
baadhi ya watanzania kudhani kuwa hawatendewi haki.

Ni vema ieleweke kuwa matukio kama haya ya uvunjaji wa amani
yasipodhibitiwa na kukomeshwa haraka yanaweza kuumba chuki ambayo
inaweza kuibua mlipuko mkubwa na machungu kwa wananchi na matokeo yake
yakawa mabaya kwa Taifa zima. Hekima na busara inatufundisha kuwa
tusipoziba ufa tutajenga ukuta.

Ni vyema wenye dhamana ya kuongoza wakakumbuka kuwa wanawajibu mbele
ya Mungu aliyewaweka au kuwaruhusu kuingia madarakani na siku moja
watatoa hesabu mbele zake.

Mwisho, natoa wito kwa watanzania wenzangu tuulinde umoja, amani na
utengamano wa taifa letu, tuikimbie dhambi ya ubaguzi kwa kuwa
tukiiruhusu itatuangamiza sote. Tuliombee taifa letu na kukiwa na
mbegu ya chuki tuimalize kwa njia ya majadiliano na vikao vya pamoja
vinavyohusisha viongozi wa dini zote na serikali pia.

Imetolewa leo 28/05/2012
Na Dk. Barnabas Mtokambali
Askofu Mkuu wa TAG

Mgombea wa Urais mrengo wa Muslim Brotherhood nchini Misri Mohammed Mursi (pichani), amesema kwamba atajumuisha makundi yote ya kisiasa katika serikali endapo atashinda duru ya pili ya Urais.

Mursi (pichani)ameahidi haya katika mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema atahakikisha kuwepo kwa uwakilishi wa wanawake na vijana.Kiongozi huyo wa chama cha Freedom and Justice amesema kwamba nia yake ni kuondoa utawala wa kiimla na kuweka msingi thabiti katika taasisi za uwongozi.

Matamshi ya Bw. Mursi yanajiri wakati afisi za hasimu wake Ahmed Shafiq zimeteketezwa na watu wanaodhaniwa wafuasi wafuasi wa makundi ya kiisilamu.

Watu wanne wamekamatwa kwa kuhusishwa na tukio hilo.Awali maelfu ya raia waliandamana nje ya makao makuu ya tume ya uchaguzi kufuatia matokeo ya raundi ya kwanza ambapo Bw Mursi alishinda kwa asilimia 24.3 dhidi ya Bw Shafiq aliyepata asili mia 23.3 ya kura.
Papa Benedict
Papa Benedict
Afisa mmoja wa ngazi ya juu katika makao makuu ya kanisa Katoliki mjini Vatican, amesema kuvuja kwa nyaraka za siri za kiongozi wa kanisa hilo duniani ni kitendo cha kikatili dhidi ya Papa Benedict. Afisa huyo ambaye ni naibu waziri wa mambo ya nje wa Vatican Angelo Becciu, amesema nyaraka hizo ni pamoja na fikra binafsi, na pia shutuma kali kutoka kwa watu waliomwandikia Papa barua za siri kutokana na nafasi yake ya kipekee.

Nyaraka hizo zinashutumu vitendo vya rushwa na kushindania madaraka katika ngazi ya juu ya Kanisa Katoliki. Hii ni kashfa kubwa kuliko zote dhidi ya Papa Benedict tangu apate wadhifa wake huo miaka saba iliyopita, na ni tukio lililochafua Kanisa Katoliki nyakati hizi. Mhudumu mkuu wa Papa, Paolo Gabriele, amekamatwa na tume ya Vatican inachunguza watu wengine ambao wamehusika katika kashfa hiyo.
It was that time of the week again that no. Housemate looks forward to. Last week, three people were put up for eviction. It’s been a stressful seven days since Mampi, Lady May and Maneta were nominated.  Tonight, Mampi was chosen to leave the House. The Zambian star had the least votes and is the first Upville Housemate to go. While the girls were getting ready half an hour before the show, Mampi said to Maneta, Prezzo and Barbz that she’s “very happy to be there but her heart is not.” Maneta then said that Mampi misses home. Do you think she’s happy and relieved to be going? The girls then put their bags downstairs, they could hear the crowd cheering next door, which made them, including us, nervous.
The show kicked off with a performance by Tanzanian hip-hop artist, Diamond. An over-eager fan jumped on stage and started dancing with the singer, but was then escorted off by security. 10 seconds later, another fan jumped up on stage, and he too was escorted. Namibian DJ, Umculo, was next to perform and presented a mix to the audience.

Big Brother presenter, IK, then switched to Upville where they could see and hear him on the screen. DKB
was asked to stand up and tell Africa who he nominated, to which he said Lady May. Lady May jumped up from the couch and said "I knew it!" She stood very confident while waving her flag. Mampi was a lot less
confident and looked very nervous as she waved to the cameras. Lady May was told that she's safe, which left Maneta and Mampi standing side by side.

IK told Maneta that she was safe, and at that moment, Mampi knew she was the one leaving. She gave the rest of the Housemates a hug and made her way out. Mampi then came onto the stage where she was interviewed by IK. The ex-Housemate said that she thinks Zainab has the potential to win because she's "crazy."

IK then turned to the random Nomination machine to see which Downville Housemates get nominated. Ghana's Keitta and Mildred were selected first. A second random Nomination was conducted, to which Botswana's Edith and Eve were selected.
Inaaminika kwamba ni idadi kubwa ya watu waliopelekwa hospitali kutokana na kujeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu Nairobi Kenya leo Moi Avenue street, ulipuaji huo wa bomu unaaminika kufanywa na kikundi cha wanamgambo wa Al Shabaab Somalia.
Jengo la pili kutoka kulia ndio lililolipuliwa, Kwa mujibu wa Nation.co.ke ni watu 30 waliojeruhiwa, polisi walikanusha kwamba sio bumu ni shoti ya umeme la shirika la umeme Kenya limekanusha kwa kusema sio shoti manake hakuna transfoma kwenye eneo la tukio ila ingekuepo ndio kungekua na uwezekano wa shoti.
Mlipuko huo ulifanya baadhi ya majengo mengine ya karibu kutingishika ambapo ulitokea kwenye saa saba na dakika kumi leo mchana, mpaka sasa haiko wazi ni wangapi wamejeruhiwa au kupoteza maisha.
HEBU mwacheni Mungu aitwe Mungu! Hatimaye habari njema kutoka katika Hospitali ya Saifee iliyopo jijini Mumbai, India anakotibiwa staa wa filamu za Kibongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ zinatia faraja kwa Watanzania.


Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa hospitalini nchini India.
Sajuki akiwa amepumzika, pembeni ni mkewe Wastara Juma.
 
ANYANYUKA KITANDANI, AONGEA
Habari hizo njema zinaeleza kuwa Sajuki aliyeambatana na mkewe, Wastara Juma na kaka yake, hatimaye ameweza kunyanyuka kitandani na kuongea tofauti na siku aliyoondoka Bongo na mwanzoni alipofikishwa hospitalini hapo. Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita kwa njia ya simu, Wastara alisema Sajuki alikuwa amepata nafuu na hali siyo mbaya kwani alikuwa na uwezo wa kuzungumza hivyo akampa simu ili azungumzie afya yake yeye mwenyewe jinsi anavyojisikia.

SAJUKI LAIVU
Sajuki alipopewa simu alianza kwa kuwashukuru wale wote wanaomuombea dua na kujitolea kwa hali na mali ili kuokoa uhai wake. “Namshukuru sana Mungu naendelea vizuri. Nilichukuliwa vipimo na nikabainika kuwa na uvimbe mwingi sehemu mbalimbali tumboni.

“Madaktari walibaini kuwepo kwa uchafu kwenye mapafu. Mwanzoni waligundua nina tatizo la kupumua na kukaukiwa damu. “Wamelishughulikia hilo kwanza na hapa nilipo nimezungukwa na madawa, kwa kweli najisikia nafuu,” alisema Sajuki kwa sauti ya kukwaruza.

MADAKTARI
Sajuki alisema alipokelewa vizuri lakini kabla ya kuanza matibabu ya uvimbe tumboni, madaktari walilazimika kumtibu kwanza tatizo la damu na pumzi hivyo matibabu ya kilichompeleka hospitalini hapo (uvimbe) yakawekwa pembeni.

WASTARA ATIA NENO
Kwa upande wake, Wastara alisema kuwa Sajuki alipaswa kupatiwa matibabu kwa wiki mbili ndipo warejee nyumbani lakini kwa hali halisi inaonekana watakaa zaidi kwani tayari wiki mbili zimekatika.

MATIBABU YAANZA
Wastara alisema kuwa baada ya kumalizika kwa tatizo la pumzi na kupungukiwa damu, madaktari wameanza vipimo vya tatizo la uvimbe na kusisitiza kuwa uzi ni uleule wa kumwombea mumewe ili arejee katika siha njema.

TUMEFIKAJE HAPA?
Sajuki alianza kusumbuliwa na uvimbe mwaka jana ulioanzia mkononi na baadaye ndani ya mwili kwenye ini na sasa madaktari wanasema siyo kwenye ini tu bali na sehemu nyingine tofauti za tumboni
 Wantazania waishio DMV Nchini Marekani wakiwa katika uzinduzi wa tawi la chadema Washington  Dc
 Uongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc  kwenye meza ya juu wa kwanza kushoto Libe Mwangombe, akifatiwa na Mhe. Peter Msigwa,  Mwenyekiti wa tawi Mhe. Kalley Pandukizi,  Mhe. Zitto Kabwe, na Mhe. Nassari Joshua, mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University Of Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.
 Mhe. Zitto Kabwe akitoa hutba kuelezea mpango mzima wa mambo yanavyoendelea nchini Tanzania