Kabila: Ntaganda akamatwe
By Maganga Media - Apr 13, 2012
| Jenerali Ntaganda anatafutwa na ICC, |
Rais Joseph Kabila amesema kiongozi wa zamani wa waasi Bosco Ntaganda, anayetafutwa na Mahakama ya Uhalifu ta ICC ni lazima akamatwe. Lakini Jenerali Ntaganda lazima yuko DRC Rais Kabila anasema.
Bw Kabila awali alikataa wito wa kumkamata mtu huyo aliyejulikana kama"The Terminator". Mahakama ya ICC kwa miaka mitano sasa inamtafuta kwa kusajili watoto kuwa askari wakati wa miaka mitano ya vita vikali DRC.
"Nataka kumkamata Bosco Ntaganda kwa sababu umati wote wa watu unataka amani," Shirika la Reuters limemukuu Rais Kabila akisema. "Amefanya uhalifu Kivu ya Kaskazini na Goma…atahukumiwa," alisema.
Mwezi uliopita mwendesha mashataka mkuu wa ICC alitaka Ntaganda akamatwe mara moja baada ya mahakama hiyo kumtia hatiani kiongozi mwingine wa waasi, Thomas Lubanga, kwa makosa kama hayo.
ICC inasema Jenerali Ntaganda alitumia askari watoto kupigana Ituri kaskazini mashariki mwaCongokuanzia mwaka 2002-2003.
Anatafutwa kwa mauaji na ubakaji.Waasi hao wa zamani haijulikani wako wapi. Anaripotiwa kuondoka Goma akichukua pamoja naye askari wenye silaha. Baadhi ya taarifa zinasema askari walioasi 600 walimbatana naye. Inaarifiwa kuwa wamechukua magari silaha na risasi na mabomu
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII