CHADEMA KUKATA RUFAA ARUSHA
By Maganga Media - Apr 9, 2012
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeamua kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa Tanzania kupinga hukumu ya kutengua matokeo ya ubunge wa Arusha Mjini wa Godbless Lema iliyotolewa katikati ya wiki na Jaji Gabriel Rwakibarila.
Akitangaza uamuzi huo katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya NMC, Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe, alisema ikiwa chama hicho kitaingia madarakani mwaka 2015 kitaondoa kinga ya kutoshitakiwa kwa viongozi wa juu wa nchi akiwamo rais, kwa madai kuwa inatumiwa vibaya. Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Arusha ulikuwa mahususi kwa ajili ya kutoa msimamo wao.
Mbowe alisema kuwa baada ya kutafakari na kushauriana na wanasheria pamoja na viongozi wenzake, waliona ni vema wakakata rufaa kwa sababu za msingi nne. Kutokana na jaji kutafsiri kuwa Lema alitukana, alibagua kijinsia na aliendesha kampeni zisizo za kistaarabu, jambo ambalo si kweli na halikutokea.
Kiongozi huyo wa kambi rasmi ya upinzani bungeni alisema kuwa kwa historia ya utoaji haki hapa nchini inaonesha kuwa haki kwenye kesi zinazowahusu wapinzani imekuwa ikipatikana kwenye Mahakama ya Rufaa hivyo ni vizuri waende kutafuta haki huko. Alisema kuwa wameamua kukata rufaa, ingawa wana uhakika wa kushinda kwa kishindo kuliko mwaka 2010, lakini wameamua kufanya hivyo ili kuokoa fedha nyingi za walipa kodi ambazo zitatumika katika kampeni.
“Kwenye Mahakama ya Rufaa baada ya kupitia hukumu ile wanaweza kuamua kumrudishia Lema ubunge wake, hivyo tukaokoa fedha za walipa kodi ambazo zinahitajika kwa ajili ya huduma za afya, elimu na mambo mengine. Hata wakiamuru uchaguzi urudiwe, bado hatuwezi kuacha kukata rufaa, kwa sababu ya wahuni wachache waliomsukuma jaji kutoa maamuzi yasiyofaa. “Nawaheshimu sana majaji lakini wao si Mungu wa kuogopwa, wanapokosea ni lazima tuwaambie ukweli, maana kuna majaji waliostaaafu na wengine bado wako kazini walinipigia simu wakatuomba tutumie busara kumaliza jambo hili kwani taifa linatutegemea, tunawaheshimu sana majaji wetu,” alisema Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, mkoani Kilimanjaro.
Hata hivyo Mbowe alisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kuziheshimu mahakama hapa nchini, kwa kile alichoeleza kuwa maamuzi ya jaji au hakimu mmoja yasichukuliwe kuwa ni ya mahakama zote, hivyo kuupaka matope mhimili wote.
Alisema kuwa CHADEMA kinapigania maendeleo ya wananchi wote na utawala wa demokrasia, hivyo kinaiheshimu mihimili yote mitatu ya dola ingawa aliitaka kuhakikisha inajiendesha kwa kufuata sheria. “ Lema alimpita mgombea wa CCM , Dk. Burian (Batilda) kwa kura zaidi ya 20,000, leo mtu mmoja anajaribu kuturudisha kwenye uchaguzi, kwa kweli kuna umuhimu mkubwa wa kuhakikisha milimili ya Bunge na Mahakama inajitegemea ili ifanye kazi kwa uhuru zaidi,” alisema Mbowe.
Hoja za mawakili
Juzi aliyekuwa wakili wa Lema na wengine wawili walibainisha kasoro nyingi za kisheria katika hukumu hiyo na kudai kuwa imetoa doa katika mhimili huo wa dola. Wakili Method Kimomogoro aliyemtetea Lema katika kesi hiyo, akidai kuwa hukumu iliyotolewa na Jaji Rwakibarila haikuzingatia hoja muhimu zaidi ya 30 alizoainisha kwenye hati yake ya majumuisho.
Alisema kuwa jaji katika hali ya kushangaza alitumia ushahidi wa wadai na mashahidi waliothibitika kuwa viongozi na wanachama wa CCM, lakini akiukataa ushahidi wa upande wa utetezi kwa hoja kuwa mashahidi walikuwa viongozi na wanachama wa CHADEMA ambao walikuwa na masilahi katika kesi hiyo.
Alisema kuwa hoja nyingine muhimu ambayo Jaji Rwakibarila hakuizungumzia wala kutolea uamuzi ni ile ya wadai kushindwa kutoa ushahidi mwingine zaidi ya ule wa kusikia ambapo awali walidai wangeleta mahakamani hapo nakala za CD zinazomwonyesha Lema akihutubia na kutoa maneno ya kashfa, udhalilishaji na ubaguzi wa kidini, lakini hawakuzileta wala hawakutoa sababu za kushindwa kufanya hivyo.
Kimomogoro alisema hoja nyingine kwamba ni ile aliyoieleza mahakama kuwa ushahidi wa kimazingira ulionesha kuwa Lema asingeweza kutoa maneno kuonyesha kuwa wanawake hawana uwezo wa kuongoza kwa sababu kwenye timu yake ya kampeni alikuwa akiongozana na wagombea udiwani wanawake ambao aliwanadi na kuwaombea kura.
Aidha, CHADEMA ilisimamisha wagombea udiwani wanawake watatu kwenye kata za Jimbo la Arusha Mjini na mgombea ubunge mwanamke katika Jimbo la Longido, ambalo wenyeji wake ni Wamasai.
Kimomogoro alisema kuwa hoja nyingine ni ile ya CCM na mgombea wake, Dk. Burian aliyedaiwa kukashifiwa kutolalamika kwenye kamati ya maadili ya jimbo licha ya kupewa fursa hiyo kisheria.
“Jaji aliacha hoja nyingi bila kuzishughulikia na kuzitolea uamuzi ndiyo maana aliweza kusoma na kumaliza hukumu yake ndani ya saa moja, licha ya ukweli kwamba mimi niliwasilisha majumuisho ya kurasa 60, mawakili wa walalamikaji walileta majumuisho yenye kurasa 30 pamoja na maelezo ya mashahidi walikuwa 18 na hoja za mawakili wa serikali ambazo kama angepitia zote ninaamini angetumia muda mrefu zaidi kutoa hukumu yake,” alieleza wakili Kimomogoro.
TANZANIA DAIMA

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII