HABARI MPYA LEO  

Wanawake Morrocco wapinga sheria ya Ubakaji

By Maganga Media - Mar 18, 2012


Wanaharakti wapinga sheria ya aibu Morocco
Wanaharakati nchini Morocco wanashinikiza serikali kufutilia mbali sheria inayowaruhusu wanaume wabakaji kuwaoa waathiwa wa kitendo hicho. Hii ni baada ya mshichana mwenye umri wa miaka 16 kujinyonga baada ya kuolewa na mbakaji wake.


Msichana huyo, Amina Filali alikunywa sumu ya kuua panya baada ya kuchapwa vikali akilazimishwa kumuoa mtu aliyembaka. Wanaharakati hao wanatumia mtandao kuendesha kampeini yao huku maandano yakipangwa kufanyika siku ya Jumamosi, kupinga sheria hiyo inayotajwa kama yenye kuaibisha.


Sheria ya nchi hiyo inawaruhusu wasichana kuolewa na  wabakaji ili waweze kuwasaidia kukwepa mahakamani. Kulingana na makundi ya wanaharakati, sheria hiyo inatumika kuidhinisha kitendo cha kitamaduni kinachoruhusu wabakaji kuwaoa waathiriwa ili kuirejeshea familia hadi yake.

http://maganga-resources.blogspot.com

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII