HABARI MPYA LEO  

MESSI Avunja rekodi

By Maganga Media - Mar 22, 2012

Lionel Messi

Mchezaji Lionel Messi ameandika historia katika klabu yake ya soka ya Barcelona katika ligi ya La Liga nchini Uhispani kwa kuwa mfungaji bora wa mabao katika historia ya klabu hiyo.

Hadi sasa Messi ameifungia Barcelona magoli 234 tangu alipoanza kuichezea klabu hiyo mwaka 2007 na hivyo amevunja rekodi ya miaka sitini iliyokuwa imewekwa na mchezaji wa zamani Cesar Rodriguez aliyefunga mabao 232 wakati akicheza katika klabu hiyo miaka ya 1950.

Messi ambaye ni raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 ametuzwa mchezaji bora duniani mara mbili mfululizo na ameifungia klabu yake mabao 54 msimu huu.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII