HABARI MPYA LEO  

Mauaji ya Afghanistan yasikitisha Marekani

By Maganga Media - Mar 14, 2012


Maiti za watu wanaoshukiwa kuuawa na mwanajeshi wa Marekani
Rais Barack Obama amesema mauaji ya raia kumi na sita wa Afghanistan yalitekelezwa na askari mmoja wa Marekani Jumapili iliyopita, yanaonyesha umuhimu a majeshi ya Marekani kuondoka nchini humo-- lakini ametahadharisha dhidi ya uamuzi wa kuharakisha kuondoka.
Bwana Obama amesema majeshi ya Marekani yataondoka Afghanistan katika utaratibu uliopangwa, ili yasiishie kurudi tena huko.

Akiulizwa kuhusu mauaji ya raia wa Afghanistan katika mahojiano ya televisheni mbalimbali za Marekani, Bwana Obama amesema mauaji hayo ni ya askari binafsi na wala sio kielelezo cha utendakazi wa majeshi ya Marekani kwa jumla.
Marekani inapanga kukabidhi shughuli za usalama kwa majeshi ya Afghanistan ifikapo mwaka 2014.
''Hatutaki kuchukua hatua za haraka. Tuna mamia ya watu wanaotupa ushauri. Tuna vifaa vingi ambavyo vinahitaji kuhamishwa...lazima tuhakikishe kwamba raia wa Afghanistan wanaweza kulinda mipaka yao na kuzuia kundi la Al Qaeda kurejea tena ..Kwa hiyo lazima tuchukue hatua kwa njia inayofaa'
Wachanganuzi wanasema tukio hilo halilitaathiri mikakati ya Marekani nchini Afghanistan.


Hata hivyo, kuchapishwa kwa picha za wanajeshi wa Marekani wakikojolea maiti za wapiganaji wa Taliban na kuchomwa kwa Quran katika kituo cha kijeshi cha Bagram kunafanya iwe vigumu kuelezea raia wa Afghanistan na hata wamarekani kwamba kuna umuhimu wa wanajeshi wa marekani kuendelea kuhudumu nchini Afghanistan.

http://maganga-resources.blogspot.com

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII