HABARI MPYA LEO  


WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imetangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu, huku idadi yao ikishuka kwa asilimia 13.34 ikilinganishwa na mwaka jana. Akitangaza majina hayo Dar es Salaam jana, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema kutokana na hatua hiyo, shule nyingi hasa zinazochukua wanafunzi wa mikondo ya sanaa na uchumi, zimekosa idadi ya wanafunzi kama ilivyotakiwa.

“Serikali ilikuwa imetenga nafasi 15,000 za wasichana, lakini waliopatikana ni 9,378 tu, nafasi zilizokuwa zimetengwa kwa wavulana ni 26,000, lakini waliopatikana ni 22,138,” alisema. Alisema wanafunzi 142 waliobakia, ufaulu wao haukuweza kutengeneza maunganisho yoyote ya masomo, kwa hiyo hawakupangwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano.

Mwaka 2010, wanafunzi 352,840 walifanya mtihani wa kidato cha nne, huku 40,388, sawa na asilimia 11.5 wakipata daraja la kwanza mpaka la tatu. Waliochaguliwa kuendelea na kidato cha tano na vyuo vya ufundi walikuwa 36,366. Mulugo alisema mwaka 2011 wanafunzi waliofanya mtihani huo walikuwa 336,301, huku 33,577 sawa na asilimia 9.98 wakipata daraja la kwanza mpaka la tatu. Ufaulu huu umepunguza idadi ya waliochaguliwa kidato cha tano na vyuo vya ufundi kutoka wanafunzi 36,366 mwaka 2011 mpaka wanafunzi 31,516 mwaka 2012. Huu ni upungufu wa wanafunzi 4,850 sawa na asilimia 13.34,” alisema Mulugo.


Mapigano mapya yamezuka kati ya majeshi ya Sudan na yale ya Sudan kusini katika maeneo kadhaa ya mipaka kati ya mataifa hayo mawili. Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini amesema mapigano hayo ndio makubwa na mabaya zaidi kuwahi kutokea tangu nchi hiyo ijipatie uhuru wake toka Sudan. Na kuchipuka kwa mapiganao hayo mapya kumemfanya Rais Salva Kiir kuonya kuwa vita vinanukia eneo hilo 

Rais Kiir amesema," asubuhi hii anga yetu ilishambuliwa kwa mabomu ....Ni katika maeneo ya Unity.
"Kiongozi huyo wa Sudan kusini amesema ni vita ambavyo wanalazimishwa kuwa navyo. Na ni Sudan ndio inatafuta vita hivyo"

Nae msemaji wa jeshi la Sudan amenukuliwa akisema kuwa vita viko katika maeneo ya South Kordofan na kusini mwa jimbo la Unity. July mwaka jana Sudan kusini ilijitenga rasmi na Sudan baada ya vita vya miaka mingi. Licha ya kujitenga huko kumekuwa na malumbano ya kisiasa na mikwaruzano kati ya nchi hizo mbili kutokana na sababu kadhaa lakini kubwa zaidi ikiwa ni zogo la mafuta. 

Radio ya kitaifa ya Sudan imetangaza kuwa Rais Omar el-Bashir amehairisha ziara yake ya kwenda Sudan Kusini. Vita hivi pia vinakuja wakati mkutano ulikuwa umepangwa kufanyika wiki ijayo kati ya Bashir na mwenzake wa Sudan Kusini ,Salva Kiir ili kusuluhisha sintofahamu kati ya nchi hizo mbili jirani
JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA


WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

MAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2012/13 

Muda wa mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 April, 2012. 

1. Kozi zinazotangazwa ni: 

A. Kozi za ngazi ya Stashahada:

(i) Afisa Afya ya Mazingira (Health Officer)
(ii) Fiziotherapia (Physiotherapy)
(iii) Fundi Sanifu Meno (Dental Laboratory Technologist)
(iv) Mteknolojia Maabara (Laboratory Technician)
(v) Optometria (Optometry)
(vi) Tabibu (Clinical Officer)
(vii) Tabibu Meno (Dental Therapist)
(viii) Uuguzi Daraja ‘’A’’ (Diploma in Nursing)
B. Kozi za ngazi ya Cheti
(i) Fundi Sanifu Maabara Msaidizi (Laboratory Assistants)
(ii) Mtunza kumbukumbu za Afya (Health Record Technicians)
(iii) Tabibu Msaidizi (Clinical Assistants)
(iv) Uuguzi Daraja ‘’B’’ (Certificate in Nursing)
C. Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya masafa ‘Distance Learning)
(i) Kozi ya Tabibu
2. Muda wa Mafunzo:
(i) Miaka mitatu (3)kwa kozi za Stashahada
(ii) Miaka miwili (2) kwa kozi za Ngazi ya cheti

3. Sifa za Muombaji:

Waombaji watarajali (Pre-service):
(i) Awe raia wa Tanzania
(ii) Awe amemaliza kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2007 na kuendelea
(iii) Ufaulu wa kidato cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’, kwa masomo ya biologia na kemia , na alama ‘D’ kwa somo la fizikia kwa kozi za Stashahada . Maksi hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mitihani.
(iv) Cheti chake cha kidato cha nne, kionyeshe ufaulu usiopungua point 28 kwa kozi za cheti. Aidha ni lazima awe na ufaulu usiopungua (minimum) alama ‘D’, kwa masomo ya biologia, Kemia na Fizikia. Maksi hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mtihani.
(v) Kwa wale waliomaliza kidato cha sita na wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya stashahada, wawe na alama isiyopungua E, kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Ufaulu huu uwe umepatikana katika kikao kimoja tu cha mtihani.
(vi) Kufaulu somo la Kiingereza na Hisabati ni sifa ya nyongeza.

Waombaji wa wanaojiendeleza (In-service) kuchukua Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya Masafa - Distance learning:

(i) Awe amemaliza kidato cha nne
(ii) Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya Waganga Wasaidizi Vijijini mwaka 1999 na kurudi nyuma.
(iii)Awe na barua ya mwajiri wake
Waombaji katika kipengele hiki watatakiwa kuchukuwa ‘Bridging course’ kwa miezi 9 na
kufaulu, ndipo waweze kuendelea na masomo ya Tabibu.

4. Utaratibu wa kutuma maombi:
(i) Fomu za maombi zitapatikana kwa wakuu wa kanda za mafunzo zilizoainishwa hapo chini (rejea kipengele Na. viii) chini, waganga wakuu wa wilaya na wakuu wa vyuo vya afya vilivyo chini ya wizara. Pia ipo kwenye mtandao - website ya wizara ya Afya www.moh.go.tz
(ii) Waombaji wote watalipia fomu kwa sh. 15, 000/=. Risiti halisi ya Benki kwa ajili ya malipo haya, itawasilishwa pamoja na fomu za maombi. Kiasi hiki cha fedha hakitarejeshwa (Non refundable).
(iii)Malipo yaingizwe kwenye akaunti ,Health Service fund’, Account No. 0111-030-12059 NBC CORPORATE BRANCH.
(iv) Maombi yatakayopokelewa na kufanyiwa kazi, ni yale yatakayoambatanishwa na risiti ya malipo ya Benki, inayoonyesha kiwango cha malipo kilichotajwa hapo juu.
(v) Maombi ambayo hayataambatanishwa na hati ya malipo ya Benki(Pay in Slip) na kivuli cha cheti cha Baraza la Mitihani cha kuhitimu Elimu ya Sekondari, hayatafanyiwa kazi.
(vi) Maombi yote yatapokelewa kupititia kanda za mafunzo baada ya malipo kufanyika kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu.
(vii) Fomu za maombi zijazwe na zitumwe kwa wakuu wa kanda kulingana na eneo ambalo muombaji alipo. Kanda ya Mashariki itakuwa na sehemu tatu za kupokelea (No. a, i na j. Anwani za wakuu wa kanda ni kama zilivyoainishwa hapa chini:-

a) Mratibu wa Kanda ya Mashariki (Mikoa ya morogoro na Pwani) - Chuo cha Mafunzo ya Afya ya Jamii S.L.P. 1060, Morogoro - (EZ)
b) Mratibu wa Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma na Tabora) Chuo cha Tabibu Wasaidizi, S.L.P. 458, Kigoma - (WZ)
c) Mratibu wa Kanda ya Kusini (Mikoa ya Lindi na Mtwara) Chuo cha Tabibu, S.L.P. 86, Mtwara - (SZ)
d) Mratibu wa Kanda ya Kaskazini (Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga) Chuo cha Mafunzo ya Walimu wa Afya, S.L.P.1162, Arusha - (NZ)
e) Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini Magharibi (Mikoa ya Rukwa na Mbeya) Chuo cha Madaktari Waasaidizi, S.L.P. 1142, Mbeya - (SWHZ)
f) Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mikoa ya Ruvuma na Iringa) Chuo cha Afya ya Jamii, S.L.P. 235, Iringa - (SHZ)
g) Mratibu wa Kanda ya Kati (Mikoa ya Singida na Dodoma) Chuo cha Uuguzi, S.L.P. 595, Dodoma - (CZ)
h) Mratibu wa Kanda ya Ziwa (Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga) Chuo cha Madaktari Wasaidizi, S.L.P. 11351, Mwanza - (LZ)
i) Mkurugenzi wa Taasisi za Sayansi Shiriki za Afya Muhimbili, S.L.P 65005, Dar-es-salaam - (EZI)
j) Mkuu wa chuo cha Tabibu, S.L.P. 30282, Kibaha - (EZK)

Mwombaji ajaze kwenye fomu ya benki kanda/chuo ambayo atapeleka fomu zake kwa kujaza herufi zilizo ndani ya mabano hapo juu, zilizoandikwa mwisho kabisa wa anuani ya kila kanda. Herufi hizo zijazwe upande wa kushoto wa fomu ya benki wakati mwombaji wanajaza mambo mengine kwenye fomu. Fomu zitapokelewa kwenye vyuo vilivyoainishwa hapo juu tu.

5. Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:
a) Wizara itakuwa na wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali kupitia magazeti, ‘website’ ya wizara na mbao za matangazo wizarani na Kanda za Mafunzo.
b) Taarifa hizo zitatumwa pia kwenye kanda za mafunzo kama zilivyoainishwa hapo juu.

6. Muda wa mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Aprili, 2012.

7. Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 1 Oktoba, 2012.

Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
S.L.P. 9083,
Dar es Salaam.

SIKU moja baada ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe kutangaza nia ya kugombea urais mwaka 2015, kauli hiyo imewachanganya watendaji wakuu wa chama hicho, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa. Wakati Dk Slaa akikosoa hatua hiyo na kusema sio wakati mwafaka sasa kuzungumzia urais, Mbowe amesema hana tatizo na Zitto kutangaza nia hiyo sasa kwa kuwa ni haki yake, lakini akahoji haraka ya kutangaza dhamira hiyo.

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti viongozi hao wamemshauri Zitto kufuata taratibu za chama kama anataka kufikia malengo yake hayo ya kutaka kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa taifa.

Kauli ya Dk Slaa
Akizungumzia uamuzi huo wa Zitto kutangaza dhamira hiyo, Dk Slaa alisema suala la urais sio muhimu kwa sasa kwani chama kinaangalia ushindi kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki. "Naomba niseme hivi, sasa urais sio ‘issue’ (suala). Chama kinaangalia uchaguzi wa Arumeru Mashariki, muda wa kuzungumzia urais ukifika, tutasema," alisema Dk slaa na kuongeza:

“…Naomba mtambue kwamba tunakabiliwa na suala kubwa la uchaguzi huku Arumeru kwa hiyo sasa siwezi kuzungumzia suala la urais, hili sio wakati wake sasa.”

Hata hivyo alimshauri Zitto kufuata taratibu kama ana nia ya kugombea urais na kufafanua kwamba, chama kina utaratibu wake na ndicho chenye uamuzi wa mwisho. “Chadema ina utaratibu wake kwa kila jambo, kama Zitto ametangaza kugombea urais 2015 huo ni uamuzi wake binafsi. Lakini mimi kama kiongozi wa chama sioni kama urais ni jambo la  kujadili wakati huu. “Ikifika wakati wakujadili masuala ya urais, tutafanya hivyo kwa undani lakini, sio kwa sasa kwani wakati wake haujafika.” 

Mbowe
Kwa upande wake Mwenyekiti Mbowe, alisema kila mtu ana busara na haki zake katika kuamua jambo na hii, ni busara yake Zitto. Lakini, Mbowe alionyesha kushangazwa na  Zitto kutangaza nia hiyo sasa wakati ambao chama kinawaza na kufikiria uchaguzi wa Arumeru Mashariki. Mbowe alisema haoni tatizo Zitto kutangaza sasa nia ya kuutaka urais kwa kuwa ni uamuzi na haki yake kwasababu kila mwanachama wa Chadema ana haki ya kuamua jambo analolitaka ili mradi afuate taratibu.

“Sioni kama Zitto ana tatizo lolote la kutangaza sasa kwamba mwaka 2015 anataka kugombea urais kwani ni haki ya kila mtu kugombea nafasi hiyo,” alisema Mbowe. Hata hivyo, alifafanua kwamba pamoja na Zitto kutangaza nia, wakati wa kuwania nafasi hiyo ndani ya chama ukifika wanachama wa Chadema ndio watakaotoa uamuzi wa nani anafaa.

Kauli ya Zitto
Jana, Zitto alipotakiwa kuzungumzia maoni ya Dk Slaa na Mbowe kuhusu uamuzi wake huo, alisema aliamua kutoa taarifa hiyo, kuondoa upotoshwaji ulikuwa ukifanywa na baadhi ya watu baada ya mjadala wake na January Makamba kuhusu umri wa Urais.

Alifafanua kuwa pamoja na kwamba ana nia ya kugombea urais, kwa sasa Chadema inachofikiria ni ushindi katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki. "Naomba niseme kuwa pamoja na kutangaza nia hiyo, hivi sasa 'focus'(mlengo) yetu ni uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki kwa kuwa lazima tulichukue jimbo," alisema Zitto.

Juzi, Zitto alituma taarifa rasmi kwenye gazeti hili akieleza nia yake ya kutaka kugombea urais mwaka 2015. “Kwanza niseme wazi kabisa kuwa urais ninautaka, nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi.”

Alitamba anao uwezo kwa kuwa ni mzalendo, mwenye utashi wa kuleta mabadiliko stahiki kulingana na nchi inavyoongozwa. Alisema mabadiliko makubwa yanahitaji  maamuzi magumu yatakayoudhi wengi hasa vigogo wa nchi za Magharibi huku akitoa mfano kuwa ni pamoja na kuzuia nchi kuuza malighafi pekee.

Alisisitiza kuwa rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi. Zitto alisema, mjadala wa umri wa kugombea urais aliouanzisha na Makamba ni mkali na kwamba baadhi ya watu kwa sababu zao binafsi, wameamua kuuita ni mjadala wake na mbunge huyo wa  Bumbuli unaowabagua wazee. 


President Barack Obama on Monday emphasized his vision for a nuclear-free world and warned that North Korea and Iran should shun nuclear weapons or face tough action from the international community. Obama, who is in Seoul for a nuclear summit, will meet his Russian and Chinese counterparts Monday.

Earlier, during a speech to students at Hankuk University in South Korea, he warned North Korea that if it moves forward with a planned test-firing of a long-range missile, it will further deepen its isolation. He said sanctions have led to the "slowing" of Tehran's nuclear program. But it remains a concern and will be a topic of discussion later with leaders of China and Russia. While the president didn't specify the course of action if Iran does not comply with international demands and produces nuclear weapons, he left little leeway for Tehran's leaders. "Iran must act with the seriousness and sense of urgency that this moment demands. Iran must meet its obligations," Obama said.

The president also directed remarks at the leaders of neighboring North Korea. He said the United States has "no hostile intent toward your country" and is "committed to peace." But Pyongyang needs to realize that years of sanctions and condemnation show that its existing nuclear strategy isn't working, Obama said, adding "there will be no more rewards for provocations." "You can continue down the road you are on, but we know where that leads," Obama said. "It leads to more of the same -- more broken dreams, more isolation, ever more distance between the people of North Korea and the dignity and opportunity they deserve."

The president ended his speech by predicting that Koreans, North and South, will someday be "united and free." "The day all Koreans yearn for will not come easily or without great sacrifice. But make no mistake, it will come. And when it does, change will unfold that once seemed impossible," he said.
Macky Sall,Mshindi wa duru ya Pili Senegal

Shirika la habari la serikali nchini Senegal limetangaza kuwa rais Abdoulaye Wade amekubali kushindwa na mpinzani wake Macky Sall katika dura ya pili ya uchaguzi wa Urais. Bwana Wade alimpigia simu mpizani wake Macky Sall, na kumuambia kuwa amekubali kushindwa. Maelfu ya wafuasi wa Macky Sall wamejitokeza katika barabara za mji wa Dakar wakisherehekea ushindi wa kiongozi wao. Mshindi huyo wa duru hiyo ya pili ya uchaguzi wa urais ameutaja ushindi wake kama muamko mpya kwa raia wa Senegal.

Macky Sall alikuwa akizungumza mara tu baada ya mpinzani wake Abdoulaye Wade mwenye umri wa 85 kukubali kuwa ameshindwa katika duru hiyo ya pili. Wade alikuwa anataka kuchaguliwa tena kama raia wa Senegal kwa muhula mwengine wa tatu baada ya kubadilisha katiba ya nchi hiyo. Mabadiliko hayo yalizua machafuko na vurugu kubwa nchini Senegal ambayo yalishtua ulimwengu kwani tofauti na jirani zake Senegali imekuwa tulivu na hajawahi kuwa na mapinduzi ya kijeshi kama jirani zake.

Lakini upinzani ulipinga hatua ya kiongozi wao mkongwe na kwenda mahakamani lakini mahakama iliidhinisha hatua ya Wade ya kubadili katiba ili aweze kusimama tena kama rais. Na baada ya dura ya kwanza kukosa kuwa na mshindi wa moja kwa moja kwani hakuna aliyepata zaidi ya asilimia 50, ikiwa ni lazima kuwe na duru ya pili ambapo viongozi wote wa upinzani walimuunga mkoni Macky Sall. Na sasa Macky Sall ambaye zamani alikuwa Waziri mkuu katika serikali ya Abdoulaye wade ameibuka mshindi.

Obama akiwa 'mpaka wa uhuru'


Rais Barack Obama akiwa ziarani Korea Kusini, amezuru eneo la mvutano la mpaka na Korea Kaskazini.Amewasili Korea Kusini kwa mkutano wa kilele kuhusu usalama wa silaha za nuklia, ikiwa sehemu ya mpango wake wa miaka minne kuzuia zana za nyuklia kufika katika mikono ya wahalifu. Akiwa nchini humo Rais Obama alizuru kituo cha ulinzi karibu na eneo linalotambuliwa na jeshi kuwa linatenga Korea Kaskazini na Kusini. Alitumia darubini kuangalia vijiji ndani ya taifa la kikoministi la Korea Kaskazini.

Hapo awali, alisimama mbele ya wanajeshi wa Marekani, na kuwaambia kuwa wako zamu kwenye "mpaka wa uhuru". Shughuli hizo alizofanya leo asubuhi, baada ya kuwasili tu Korea Kusini, zimekusudiwa kuwaunga mkono wanajeshi wa Marekani walioko huko na kuonesha ushirikiano wa kijeshi baina ya Marekani na Korea Kusini. Pia zinaonesha mvutano ulioko hivi sasa na Korea Kaskazini yenye silaha za nyuklia.

Korea Kaskazini haitahudhuria mkutano huo wa kilele mjini Seoul. Mazungumzo nje ya mkutano yanaelekea kuhusika hasa na hitilafu mpya kati ya Marekani na Korea Kaskazini, kuhusu mpango wa Korea Kaskazini kurusha satalaiti angani mwezi ujao. Wakuu wa Marekani wamesema wazi kuwa Rais Obama atalipeleka swala hilo kwenye mazungumzo yake na marais wa Uchina na Urusi.

Maganga Media
OBAMA at Nuclear security summit in South Korea
 
President Barack Obama used his first visit to the demilitarized zone that splits the Korean peninsula to peer through binoculars into North Korea where flags flew at half-staff to mark the 100-day anniversary of the death of Kim Jong Il. The stop at the border Sunday marked the start of a three-day trip to South Korea where the American president is to attend an international nuclear summit.

Top officials from 54 countries including China and Russia will attend the summit. But its message of international cooperation has been overshadowed by North Korea's announcement last week that it is planning to carry out a rocket-powered satellite launch in April. Obama's visit to the demilitarized zone was to meet with some of the 28,500 U.S. troops stationed in South Korea. But the stop also appears to have been intended as a message to North Korea's new leader, Kim Jong Un, that the United States remains committed to South Korea and in its standoff with the country over its development of nuclear power.

"When you think about the transformation that has taken place in South Korea during my lifetime, it is directly attributable to this long line of soldiers, sailors, airmen, Marines, Coast Guardsmen who were willing to create the space and the opportunity for freedom and prosperity," Obama told troops at a base near the DMZ. "And the contrast between South Korea and North Korea could not be clearer, could not be starker, both in terms of freedom but also in terms of prosperity."

It was Obama's first trip to the demilitarized zone, though he has made two previous trips to South Korea as president. Secretary of State Hillary Clinton paid a visit to the area in 2010. Across the border, North Koreans were mourning the death of Kim. Kim's son, who took over from his father following his death in December, and senior party officials visited the Kumsusan Palace of the Sun in Pyongyang to observe a moment of silence, said North Korea's state-run Korean Central News Agency (KCNA).

The palace serves as the burial site for Kim Il-sung, the founder of North Korea, and his son, Kim, who succeeded him as the country's ruler.

In South Korea, Obama is expected to hold a bilateral meeting with his Seoul counterpart Lee Myung-bak.
President Lee has already said he will use the summit to drum up international support against the actions of his northern neighbor.

South Korea has said it considers the satellite launch an attempt to develop a nuclear-armed missile, while the United States has warned the move would jeopardize a food-aid agreement reached with Pyongyang in early March.

North Korea says it has a right to a peaceful space program and has invited international space experts and journalists to witness the launch. KCNA cited a spokesman from the Secretariat of the Committee for the Peaceful Reunification of Korea as denouncing the South for working to turn the summit "into a platform for (an) international smear campaign" against the North. Seoul's nuclear summit will be the second after Obama hosted the first meeting in Washington in 2010. He initiated the biennial summit after presenting his vision of a nuclear-free world in Prague in April 2009.

The official agenda will deal with nuclear terrorism and how to secure the world's nuclear material.
Although North Korea is not on the agenda, it is likely to be discussed on the sidelines. Pyongyang announced this month it would carry out a "satellite launch" in mid-April to commemorate the centenary of the birth of Kim Il Sung, the country's founder.

Using ballistic missile technology, however, is in violation of U.N. Security Council Resolution 1874 and against a deal struck with the United States earlier this month that it would not carry out nuclear or missile tests in return for food aid. Pyongyang has said it will see any critical statement of its nuclear program as "a declaration of war."

Concerns about Iran's nuclear program, again not on the official agenda, will also be discussed in bilateral meetings between leaders. The date of Obama's visit "is virtually two years to the day" since the sinking of the South Korean warship, the Cheonan, which left 46 Southern sailors dead, said Daniel Russel, director for Japan, South Korea, and North Korea at the U.S. National Security Council.

South Korea says a North Korean torpedo attack was to blame for the ship's sinking. The North has denied the accusation.

SOURCE: CNN
Maganga Media

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani,Papa Benedict xvi
Akiwa ziarani nchini Mexico, Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedict wa 16 ametoa wito kwa jamii kuwajali na kuwalinda watoto sambamba na kutuma ujumbe maalumu kwa kundi lililoathirika baada ya ghasia. Huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia papa Benedict wa 16 alitaja kashfa ya matendo mabaya dhidi ya watoto inayomuhusisha kuhani wa katoliki katika kipindi cha hivi karibuni.

Hii ni ziara ya pili kwa kiongozi huyo kutembelea bara lenye idadi kubwa ya wakatoliki duniani akisisitiza kupiga vita matumizi ya madawa ya kulevya na vitendo viovu dhidi ya ubinadamu.
Katika ziara yake kiongozi huyo wa katoliki duniani anatarajia kujadili mambo mbalimbali na raisi Felipe Caldero ikiwemo masuala ya uhalifu uliokithiri pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.

Papa amesema yeye ni mgeni wa kuleta matumaini. Amesema anataka kuwasaidia Wamexico kubadilisha maisha yao, na amelaani ghasia zinazohusika na madawa ya kulevya, ambazo zimeuwa maelfu ya wananchi katika miaka ya karibuni.


Maganga Media
Zitto Kabwe, Naibu katibu mkuu CHADEMA
 
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Zitto Kabwe ameibuka na kusema kuwa anataka kuwa rais wa Tanzania mwaka 2015.Wakati Zitto akitoa kauli hiyo nzito, Waziri  wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta naye amesema anashangazwa na watu wanaoweweseka wanaposikia kuwa mwanasiasa huyo anayeongoza vita dhidi ya ufisadi ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, anataka kuwania urais.

Kauli hiyo ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni huenda ikaibua mjadala mzito ndani ya chama chake, ukiacha zile mbio za vigogo wa CCM wanaotajwa kuutaka urais 2015. 

Katika taarifa yake aliyoituma jana kwa gazeti la Mwananchi Jumapili, Zitto alisema; “ Kwanza niseme wazi kabisa kuwa Urais ninautaka, nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi.”  Alitamba anao uwezo kwa kuwa ni mzalendo, mwenye utashi wa kuleta mabadiliko stahiki kulingana na nchi inavyoongozwa.   Katika taarifa hiyo ameeleza kuwa kwa sasa nchi imesahau maendeleo ya watu badala yake imejikita katika maendeleo ya vitu.

 “Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo badala ya mambo ya msingi,” Zitto amesema taarifa na kuongeza:   “Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika, ninajua nchi yetu inahitaji uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa badala ya mabadiliko ya juujuu.”  Alieleza kuwa mabadiliko makubwa  yanahitaji  maamuzi magumu yatakayoudhi wengi hasa vigogo wa nchi za Magharibi huku akitoa mfano kuwa ni pamoja na kuzuia nchi kuuza malighafi pekee.   Alisisitiza kuwa rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma ndio kikwazo kikubwa cha maendeleo ya nchi na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi.  

“Rasilimali kama madini, mafuta, gesi asilia, ardhi na nyinginezo ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.  Sababu za kutaka  Urais  Katika taarifa hiyo Zitto alieleza kuwa kwa sasa nchi inahitaji kiongozi wa juu atakayekabili changamoto muhimu na kwamba yeye anaweza kuwaongoza Watanzania kukabiliana na changamoto hizo.  “Sio kazi rahisi, lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye, mimi nataka kuifanya, nina uwezo wa kuifanya,” alitamba katika taarifa hiyo.
 

Samwel Sitta 
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amevunja ukimya na kutema cheche kuhusu suala la kugombea urais katika uchaguzi wa 2015 na kusema kuwa wanaomkataza kuzungumzia suala hilo wameingiwa kiwewe.Sitta ambaye amekuwa akitajwa kuonyesha nia ya kuwania nafasi hiyo, amesema itakapofika wakati wa kutangaza nia yake hakuna mtu atakayemzuia.

Alisema hayo wakati akifungua Bonanza la Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana, lililofanyika Msasani Beach. "Linapoingia suala la Urais kuna watu wanapata kiwewe, wanaposikia ninataka kugombea, lakini hiyo ni haki ya kila Mtanzania mwenye sifa anaruhusiwa kugombea," alisema Sitta. Alisema muda utakapowadia wa yeye kufanya hivyo, hakuna atakayemzuia kugombea nafasi hiyo kwa sababu atakuwa anatumia haki yake kikatiba.

Alisema kuna baadhi ya watu wanatumia vibaya maneno ya Rais Jakaya Kikwete kwa kueleza kiongozi atakayemfuata lazima awe kijana, kitu ambacho Sitta alisema kamwe Rais hakumaanisha hivyo. Alisema Watanzania wamechoshwa kila siku kusikia habari za rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma na kusababisha gharama za ujenzi wa miradi mbalimbali kuwa juu kwa manufaa ya watu wachache.

Maganga Media

 CHANZO: Gazeti la MWANANCHI
  • Uhalifu na wizi wa bidhaa wakithiri

  • Waasi wa Tuareg waendeleza mashambulizi Kaskazini mwa Mali.

  • Umoja wa Ulaya waiwekea vikwazo Mali

    Mapinduzi ya Mali


    Ikiwa leo ni siku ya tatu tangu jeshi la Mali lifanye mapinduzi, Kepteni Amadou Sanogo, kiongozi wa mapinduzi, ametokeza kwenye Televisheni ya taifa kuomba msamaha kwa wizi wa ngawira unaofanywa na wanajeshi wa daraja za chini, na wale aliowaita watu wasiokuwa na nia njema. Alisema vitendo hivyo siyo kazi wala azma yao. 

    Kepteni Sanogo piya alikanusha tetesi kwamba aliuliwa jana usiku, na kwamba njama nyengine ya mapinduzi inapikwa na wanajeshi watiifu kwa Rais Amadou Toumani Toure. Inaelekea maafisa wa vikosi vengine vya jeshi walikuwa wamemzunguka Kepteni Sanogo wakati wa hotuba yake hiyo kwenye televisheni, kuonesha kuwa jeshi liko pamoja na linaunga mkono mapinduzi hayo. 

    Inafikiriwa kuwa Rais Toure bado analindwa na kikosi maalumu na hakuna hakika kuwa jeshi zima sasa linamuunga mkono kiongozi mpya. Muungano wa vyama vikuu vya upinzani, umelaani mapinduzi hayo, na umetaka uchaguzi ufanywe. Uchaguzi ukitarajiwa kufanywa mwisho wa mwezi huu.

    MALI YAWEKEWA VIKWAZO
    Mawaziri wa Mambo ya Nje ya Umoja wa Umoja wa Ulaya wameiwekea vikwazo vya kiuchumi Mali kufuatia mapinduzi ya kijeshi ikiwa ni hatua mojawapo ya kushinikiza kurejeshwa kwa utawala wa kiraia nchini humo. Uamuzi huo umefikiwa mjini Brussels kufuatia kikao kilichofanywa na mawaziri hao siku ya Ijumaa Machi 23 mwaka huu. Kwenye tamko lao la pamoja mawaziri hao wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya walilaani vikali kitendo kilichofanyywa na wanajeshi wa Mali na kuwataka kusitisha mapigano mara moja. 

    Tamko hilo pia limejumuisha amri ya kuwataka wanajeshi hao kuwaachia huru maafisa wa serikali wanaowashikilia akiwemo aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Amadou Touman Toure. Kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyofanywa nchini Mali, nimeamua kusitisha kwa muda shughuli zote za maendeleo zinazofanywa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya nchini humo hadi hapo hali itakaporejea na kuwa kama inavyotakiwa." alisema Kamishna wa Masuala ya Maendeleo wa umoja huo Andris Piebalgs.

    Kikosi cha jeshi la waasi wa Mali


    Wakati vikwazo vya kiuchumi vikianza kuiandama Mali, huko Bamako mji mkuu wa nchi hiyo Kiongozi wa mapinduzi hayo kijeshi Kapteni Amadou Sanogo ametangaza mpango wa kuwapeleka mahakamani Rais wa nchi hiyo na viongozi wake wa juu ambao wanawashikilia hadi sasa. Pamoja na nia hiyo ya kuwafikisha katika mikono ya sheria viongozi hao, Kapteni Sanogo pia amezungumzia kuhusu usalama wa watu hao na kusema kuwa wako hai chini ya uangalizi mzuri.

    "Hawa watu wako salama salimini. Hatutawagusa hata nywele vichwani mwao. Nitawafikisha mahakani ili watu wa Mali wapate kuufahamu ukweli." Alisema Kapteni Amadou Sanogo katika mahojiano na Shirika la Habari la Ufaransa AFP katika kambi ya kijeshi karibu na mji mkuu wa nchi hiyo. Hata hivyo umoja huo umesisitiza kuwa bado utaendelea kuwasaidia raia wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa misaada ya moja kwa moja ya kibinaadamu. Mali inakabiliwa na tishio la baa la njaa kufuatia kukumbwa na ukame. Baraza la Umoja wa Ulaya lilipanga kutumia kiasi cha Euro milioni milioni 583 kwa ajili ya shughuli za maendeleo nchini Mali katika kipindi cha mwaka 2008 na 2013.

    mashambulizi zaidi

    Waasi wa Tuareg nchini Mali wameendeleza mashambulizi Kaskazini mwa nchi hiyo wakati huu ambapo askari hao waasi wanakosolewa na ulimwengu kwa kufanya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali kwa madai ya serikali kushindwa kumaliza mapigano nchini humo.

    waasi wa kundi la Tuareg waliofanya mapinduzi ya kijeshi nchini Mali
    waasi wa kundi la Tuareg waliofanya mapinduzi ya kijeshi nchini Mali

     Umoja wa Afrika AU umeisimamisha Mali kwa muda katika umoja huo, wakati Ulaya imesitisha misaada na Marekani imetishia kufanya hivyo huku kukiwa na mfululizo wa matamko ya kukosoa mapinduzi hayo ya kijeshi katika nchi hiyo kinara katika mapambano ya usafirishaji wa dawa za kulevya.
    Mapinduzi hayo yamefungua njia kwa waasi hao wa Tuareg kuimarisha udhibiti wa eneo la Kaskazini huku kundi lao la harakati za kitaifa za ukombozi wa Azawadi MNLA likisema kuwa wameuteka mji wa Anefis ulioko katikati mwa miji muhimu ya Gao na Kidal.


    Maganga Media
    Rais mpya wa Ujerumani, Joachim Gauck (Kulia) akiapa leo


    Siku 5 baada ya kuchaguliwa kuwa rais mpya wa Ujerumani,Joachim Gauck ameapishwa rasmi mbele ya wabunge wa mabaraza yote mawili,bunge la shirikisho Bundetag na baraza la wawakilishi wa majimbo Bunderat mjini Berlin. Spika wa bunge la shirikisho Bwana Norbert Lammert alifungua hafla hiyo maalum .Spika wa bunge amesema kuchaguliwa Gauck ni ushahidi wa maendeleo katika kukuwa pamoja wakaazi wa mashariki na magharibi ya Ujerumani.

    Spika wa baraza la wawakilishi wa majimbo Bundesrat Horst Seehoffer amesema kuchaguliwa Joachim Gauck ni hatua muhimu katika historia ya Ujerumani."Mwanatheolojia wa Mashariki alikuwa mstari wa mbele katika mapinduzi ya amani ya mwaka 1989 katika Ujerumani mashariki ya zamani,amesema mwenekiti huyo wa chama cha kihafidhina cha CSU aliyeidaka kauli mbiu ya wakati ule "Wananchi ni sisi".


    Maganga Media

    Baada ya jeshi la Mali kutangaza kuipindua serikali ya rais Amadou Toumani Toure, kumekuwa na shutma za kimataifa dhidi ya wanajeshi hao. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limetaka utawala wa kikatiba kurejeshwa nchini humo, huku Benki ya Dunia pamoja na Benki ya Maendeleo barani Afrika wakisema wanasitisha baadhi ya shughuli nchini humo.

    Msemaji wa wanajeshi waasi nchini Mali amesema jeshi litarejesha demokrasia nchini humo na kuwa umoja utarejea hivi karibuni. Kufikia sasa haijulikani alipo Rais Amadou Toumani Toure, lakini taarifa ya televisheni ya taifa ilisema kuwa rais huyo yuko katika hali nzuri ya kiafya.

    Sababu kuu ya wanajeshi hao kuasi na hatimaye kuchukuwa madaraka ya nchi, ni kile walichokiona kama ulegevu wa serikali katika suala la vita dhidi ya waasi wa Toureg, kaskazini mwa nchi hiyo. Kwa kipindi sasa, wanajeshi walikuwa wakilalamikia upungufu wa vifaa vinavyotolewa na serikali kupambana na waasi hao, ambapo mapigano makali katika miezi ya hivi karibuni yamegharimu maisha ya watu kadhaa na kuwalazimisha takribani raia 200,000 kuzikimbia nyumba zao.

    Mwezi uliopita mamia ya watu waliandamana katika mji mkuu, Bamako, kuilalamikia serikali kushindwa kuwadhibiti waasi wa Toureg, ambao wengi wao wana silaha kutoka serikali ya zamani ya Libya, chini ya Marehemu Muammar Gaddafi.


    Maganga Media
    Waziri mkuu aliyejiuzuru, Edward Lowassa

    KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amemtaka Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa kueleza jinsi alivyoshughulikia kutatua tatizo la ajira wakati akiwa Waziri Mkuu. Kauli hiyo ya Nnauye inakuja siku moja baada ya Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka kueleza kwamba tatizo hilo haliwezi kufafanishwa na bomu na kufafanua kuwa wanaosambaza uvumi huo hawaitendei haki Serikali.

    “Kila siku wanalalamika Serikali ya CCM inatengeneza bomu katika suala la ajira, lakini hao wanaolalamika si walikuamo madarakani na  walifanya nini. “Unapofika wakati unazungumzia masuala yanayogusa jamii na Taifa kwa ujumla unapaswa kuwa na  uhakikika na unachokisema sio kupita katika makanisa kuongea kitu ambacho huna uhakika. “Amekuwa akitumia njia mbalimbali hususan makanisani kuelezea tatizo la ajira ambalo linaitatiza serikali, lakini mimi nabaki na msimamo ule ule kuwa  yeye alipokuwa serikalini (Waziri Mkuu) alifanya nini kutatua tatizo la ajira,” alihoji tena.

    Tucta
    Katibu Mkuu wa Chama cha wafanyakazi (Tucta), Nicolas Mgaya alisema suala la ajira bado ni tatizo  kwa serikali na kwamba linapaswa kutatuliwa. Mgaya alisema kuna vijana wengi wanahitimu masomo katika kila fani kwamba kupata kazi ni tatizo ambalo kama litasimamiwa ipasavyo litapungua.

    Mgaya alisema serikalini kuna upungufu wa wafanyakazi, lakini inashindwa kuajiri,  sasa umefika wakati wa kuziba mapengo hayo na kuwaondoa vijana walioko mitaani bila ajira. “Katika shule za msingi na sekondari kuna upungufu wa walimu, lakini majumbani kwetu kuna vijana waliohitimu masomo ya ualimu hawajaajiriwa sasa hapa serikali inataka kutatua ama inaongeza matatizo,” alihoji Mgaya.

    CHANZO: Mwananchi

    Maganga Media
    Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Kampuni ya Mwananchi Communication, Profesa Palamagamba Kabudi akimkaribisha ofisini Mkurugenzi Mtendaji mpya wa MCL Tido Mhando, katikati ni Mhariri Mtendaji wa kampuni hiyo Theophil Makunga


    BODI ya Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), imemteua Mwandishi wa Habari Mkongwe barani Afrika, Tido Mhando kuwa Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo kuanzia jana.
    Maganga Media
    Mohamed Merah

    Mshukiwa wa mauji ya watu wanne katika shule ya Kiyahudi mjini Toulouse Kusini mwa Ufaransa  siku ya Jumatatu Mohammed Merah ameuawa katika makabiliano na polisi katika makaazi yake. Polisi walivamia nyumba ya mshukiwa huyu baada ya harakati zao za kumtaka Merah mwenye umri wa miaka 23 raia wa Ufaransa mwenye asili ya Algeria kujisalimisha kutofua dafu kwa saa 32.Waziri wa mambo ya ndani Claude Gueant amesema mshukiwa huyo alikuwa amejificha bafuni na alipowaona polisi alianza kuwafwatulia risasi kabla ya kuruka dirishani na alipatikana akiwa ameuawa baada ya kuanguka chini.


    Katika makabiliano hayo, polisi watatu walijeruhiwa  mmoja akipata majeraha mabaya  mguuni na kukimbizwa hospitalini kupata matibabu. Mshukiwa huyo alikiri kuwa mwanamgambo wa Al-Qaeda aliyepata mafunzo kutoka Pakistan na Afganistan alituhumiwa pia kuwaua wanajeshi watatu Kusini mwa nchi hiyo wiki mbili zilizopita,mauji ambayo alisema alitekeleza kutokana na majeshi ya Ufaransa kuwa nchini Afganistan. Polisi waliamua kuvamia makaazi yake baada ya kupoteza mawasiliano naye usiku kucha na walitumia milipuko kadhaa kumtisha ili ajisalimishe kwao bila mafanikio.

    Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkzoy amesema kila juhudi zilifanywa  kumkamata Merah akiwa mzima ili afunguliwe mashtaka na kuonya kuwa serikali yake inaendelea kufanya uchunguzi zaidi ya ugaidi hasa kwa wale wanotumia mitandao na wanaosafiri katika nchi za kigeni kupata mafunzo ya kigaidi. Kiongozi wa mashtaka Francois Molins amesema Merah apigwa risasi kichwani wakati akiruka dirishani,na pia alipiga picha na kuchukua video alivyotekeleza  mauji ya watoto watatu na mwalimu wao katika shule ya Kiyahudi siku ya Jumapili.

    Kuuawa kwa mshukiwa huyo kunatamatisha oparesheni  hiyo ya siku mbili ya kujaribu kumkamata  baada ya kutekeleza mauji ya watu saba.


     CHANZO: RFI

    Maganga Media
    Sepp Blatter rais wa shirikisho la soka duniani duniani FIFA

    Rais was shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesema shirikisho hilo litahakikisha kuwa wachezaji wote wanapata bima ya afya  wakati wanapocheza katika mechi zote za kimataifa. Blatter amewaambia wajumbe wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA kuwa,vyama vya soka kote duniani vitatia saini makubaliano hayo kufikia mwezi Mei mwaka huu.


    Wachezaji watakaonufaika na mpango huo ni wale wote watakaochezea timu zao za taifa na vlabu katika mechi zote zinazotambuliwa na FIFA. Tayari shirikisho la soka barani Ulaya Uefa, limetangaza kuwa litaanza zoezi la kutoa bima kwa wachezaji wote wakati wa michuano ya bara Ulaya  baadaye mwaka huu.

    Maganga Media