Naibu jaji mkuu wa Kenya apatikana na hatia
By Mhariri - Aug 6, 2012
Jopo maalum la majaji lililoteuliwa na rais Mwai Kibaki kuchunguza tuhuma zilizokuwa zinamkabili Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Nancy Baraza kumdhalilisha mlinzi mmoja katika duka moja kubwa mjini Nairobi, imependekeza, jaji huyo kuondolewa madarakani.
Amesema kitendo alichofanya Nancy Baraza na ni cha utomvu mkubwa wa nidhamu na hivyo kupendekeza kwa Rais Mwai Kibaki kumwondoa katika wadhifa wake wa naibu jaji mkuu. Nancy Baraza alituhumiwa kumnyanyasa na kumpiga Bi Kerubo tarehe 31 Desemba 2011, baada ya kutakiwa kufanyiwa ukaguzi kabla ya kuingia katika duka hilo, utaratibu ambao umekuwa ukitekelezwa kwa wateja wote.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII