Wafungwa Malawi wacharuka!
By Unknown - Jul 8, 2012
Rais Joyce Banda, siku ya Ijumaa aliwasamehe wafungwa karibu 400, lakini siyo wale waliofungwa kwa sababu ya mauaji au ubakaji.
Wafungwa katika gereza ya Zomba, mashariki mwa nchi, walitoroka kwenye seli zao na kuwabughudhi wasimamizi, wakisema wafungwa wawili waliosamehewa ni wahalifu wa mauaji na ubakaji.
Bibi Banda alisema wabakaji wanafaa kufa jela, hasa wale waliowabaka watoto. Ubakaji wa aina hiyo unatokea mara kadha Malawi, kwa sababu kuna wanaoamini kuwa kufanya mapenzi na msichana bikira kunaleta mali na kunatibu HIV na UKIMWI.
KUTOKA BBC
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII