Morsi akaidi amri ya jeshi
By Unknown - Jul 8, 2012
Katika hatua ya kulikaidi jeshi lenye nguvu nchini Misri, rais mpya Mohammed Morsi, ametoa amri kuwa bunge likutane.
Amri yake inakwenda kinyume na hukumu iliyotolewa mwezi uliopita na mahakama ya katiba, kwamba bunge la sasa siyo halali. Bunge hilo lina wajumbe wengi wa vyama vya Kiislamu.
Hukumu ya mahakama ilitekelezwa na jeshi, ambalo lilifuta bunge na kujipa madaraka ya kutunga sheria. Televisheni ya taifa inasema halmashauri ya jeshi itafanya kikao cha dharura kujadili amri ya Rais Morsi.
SOURCE: BBC
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII