Uteuzi wa Msajili Mkuu wa Mahakama
By Unknown - Jul 7, 2012
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Ignus Paul Kitusi kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama (Chief Registrar) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012. Kabla ya kuteuliwa kushika wadhfa huo mpya, Bwana Kitusi alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu.
Katika uteuzi huo, vilevile Rais Kikwete amemteua aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Rufani la Kodi, Bwana Panterine Muliisa Kente kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani (Registrar of the Court of Appeal) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.
Aidha, Mhe. Rais amemteua Bwana Benedict Bartholomew Mwingwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu (Registrar of the High Court) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012. Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mwingwa alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Julai, 2012
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII