Rais mpya wa Ghana!
By Unknown - Jul 25, 2012

John Mahama.
Kuhusu chanzo cha kifo cha Mills, BBC wamesema taarifa kutoka ofisi ya rais zinasema alifariki ghafla baada ya kupelekwa hospitali Jumatatu usiku na inaaminika aliugua ugonjwa wa kansa.
Kifo cha rais wa taifa hilo la pili duniani kwa ukuzaji wa cocoa kimekuja wakati alikuwa anajiandaa kugombea tena urais.

Ghana ilikuwa inatarajiwa kwenda katika uchaguzi mkuu Disemba mwaka huu ambapo John Attah Mills alikuwa ametangaza nia yake ya kutetea hiyo nafasi, wakati wa uongozi wake, uchumi wa Ghana uliimarika na demokrasia kupanuka zaidi.
John Atta Mills ambae alianzisha uchimbaji wa mafuta nchini Ghana amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 68 na amefariki dunia siku tatu tu baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa July 21.
Kwa hisani ya Millard Ayo
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII