Mama Lwakatare alia na mavazi ya aibu
By Unknown - Jul 24, 2012
Mchungaji Kiongozi wa kanisa la Mikocheni Assemblies of God la jijini Dar es Salaam na mbunge wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dk Getruda Lwakatare, akichangia hoja ya makadirio ya bajeti ya mapato na matumizi ya wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mwaka wa fedha 2012/2013.
Akichangia hotuba hiyo alionesha hisia zake kutopenda uvaaji wa mavazi ya vitopu na vipedo katika maeneo mbalimbali ya jijini Dar es Salaam kama vile Posta, Kariakoo, na mikoani kuwa ni aibu hivyo serikali iwe na sheria kali dhidi ya wavaaji wa mavazi hayo. Mathalani amesema kuwa baadhi ya wanawake wana maumbo makubwa na hivyo kuendelea kuvaa mavazi hayo ni kujivua utu wao.
Kuhusu kanga moko, amelaani mchezo huo ambapo kwa maelezo yake licha ya kuwa ni kanga moja bado inakuwa imelowanishwa maji kitu ambacho ni kitendo cha aibu.
Pia ameongelea kuhusu vipindi vya runinga na redio visivyozingatia maadili na wala visivyo na mafunzo kuutumia muda huo kwa wataalamu mbalimbali kama wa afya kutoa mafundisho dhidi ya afya ya uzazi, UKIMWI, nk ikizingatiwa kuwa vijana wengi hawana utaratibu wa kusoma vitabu hivyo itakuwa vizuri zaidi wakisikia na kuona kwa wakati mmoja.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII