HABARI MPYA LEO  

Mafuriko yauwa 35 Nigeria

By Unknown - Jul 25, 2012

Watu wapatao 35 wamekufa kufuatia mafuriko yaliyotokea katikati mwa Nigeria baada ya mvua kubwa na kusababisha bwawa kufurika karibu na mji wa Jos.

Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu katika eneo hilo amesema nyumba zipatazo mia mbili, nyingi zikiwa zimejengwa kwa udongo zimezama au kuharibiwa na mafuriko.

Taarifa zinazohusiana.Maafisa wanasema watu wapatao ishirini na watano hawajulikani walipo na kwamba idadi ya watu waliokufa inatarajiwa kuongezeka. Shirika la Taifa la Kushughulikia Majanga limeanza operesheni ya misaada ya dharura. Mtu mmoja alinukuliwa akisema kuwa amewapoteza watoto wake saba katika mkasa huo.

Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu katika Jimbo la Plateau amesema miongoni mwa waliofariki ni mzee wa miaka 90.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII