HABARI MPYA LEO  

Uhalifu dhidi ya Binadamu Syria

By Maganga Media - Jun 2, 2012


Syria moto
Mauwaji ya zaidi ya raia 100 katika mji wa Houla nchini Syria wiki iliyopita huenda ukaelezewa kama uhalifu dhidi ya binadamu, kwa mujibu wa Kamishna wa Haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa. Navi Pillay ameisihi jumuia ya kimataifa itumie kila njia na juhudi kuhakikisha wahusika wa vitendo hivyo wanawajibika.
Bw.Pillay aliyasema haya wakati akihutubia Kikao cha dharura cha Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.
Hapo awali, wanaharakati wa upinzani walisema kua kuna mauwaji mengine ya raia yaliyofanywa na wana mgambo wanaoungwa mkono na serikali.

Mauwaji Syria
Mauwaji Syria
Wafanyakazi 13 wa kiwanda kimoja waliamrishwa kutoka ndani ya basi walilokua wakisafiria na kuuawa na ''Shabiha'' Jina la wanamgambo hao wanaoiunga mkono serikali siku ya alhamisi huko al Buwaida al Sharkiya, karibu na mji ulio magharibi mwa nchi wa Qusair.

Video kadhaa zilizotumwa kupitia mtandao zilionyesha maiti zenye majeraha ya risasi zilizopigwa kichwani na kwenye tumbo, ikiashiria walipigwa risasi na mtu aliye karibu nao.

Madai hayo ya wanaharakati hayana uthibitisho huru, lakini wasimamizi wa Umoja wa Mataifa walioko huko Syria waliweza kuthibitisha madai kama haya mara mbili katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, likiwa ndilo shirika la kiwango cha juu duniani, lilianza mkutano wa dharura kujadili ghasia za nchini Syria. Hii ni mara ya nne kwa Baraza hili kujadili Syria tangu vuguvugu la kumpinga Rais Bashar Al Assad lianze mnamo mwezi Machi mwaka 2011.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII