NIDO yasherehekea siku ya Maziwa Duniani na watoto yatima
By Maganga Media - Jun 2, 2012
Meneja wa Sayansi na Uthibiti wa Nestle Tanzania Akikabizi zawadi kwa watoto wa kituo cha kulelea watoto cha Chakuwama Orphanage Centre kama Sehemu ya Kusheherekea siku ya Maziwa Duniani, Pamoja na watoto hao Pembeni ni Mlezi wa Kituo pamoja na maofisa wakuu wa Biashara Kutoka Kampuni ya Nestle Tanzania.
Mlezi wa kituo cha Kulea watoto yatima cha Tanzania Mitindo House na Mwanamitindo Maarufu Bi Khadija Mwanamboka akiojiwa na waandishi wa habari wakati akipokea zawadi kwa ajili ya kituo cha watoto yatima cha TMH ambapo Kampuni ya Nestle kupitia bidhaa ya NIDO imewawezesha vituo vitatu vya watuto yatima vya Dar es Salaam kusherehekea Siku ya Maziwa Dunia kwa kuwapa Maziwa ya NIDO na Bidhaa ya MILO zenye thamani zaidi ya TSZ 5 Milioni.
Bibi Mlezi wa Kituo cha CHAKUWAMA Bi. Khadija alipokuwa akihojiwa na Muandishi wa Habari wa ITV Bw. Sam Mahele Juu ya Changamoto wanazozipata katika harakati za uendeshaji wa Vituo vya watoto yatima pamoja na Michango ya Taasisi mbalimbali kama Kampuni ya Nestle NIDO ilivyofanya kuwawezesha watoto kuwa na afya bora na kuhamasisha Unywaji wa Maziwa hali Ng’ombe yaliokatika mifumo mbali mbali.
Bidhaa za NIDO, CereVita, MILO kutoka Kampuni ya Kubwa ya Vyakula na Vinywaji Dunia ya Nestle zenye thamani ya TZS 5,548,800 Zilizogawiwa kwa vituo vya Umra, Chakuwama na Tanzania Mitindo house zenye watoto takribani 200 wanaolelewa na vituo hivyo katika kuazimisha siku ya Maziwa Duniani ambayo hufanyika kila mwaka Juni 1st.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Nestle Tanzania wakionyesha furaha yao baada ya Kujumuika na watoto wa Vituo vya watoto yatima na kuchangia Vyakula kwa ajiri ya kuboresha afya na maisha ya watoto hao kama sehemu ya kurudisha kwa jamii kwa kampuni hiyo wakati wakisheherekea siku ya Maziwa Duniani Juni Mosi ya Kila Mwaka.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII