HABARI MPYA LEO  

TENDWA: Mkapa na Vicent acheni uchochezi!

By Maganga Media - Mar 17, 2012

Msajiri wa Vyama Vya Siasa nchini, John Tendwa


MSAJILI wa Vyama Vya Siasa nchini, John Tendwa ameelezea kukerwa na malumbano ya Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Mbunge wa Musoma mjini (Chadema), Vincent Nyerere na kuonya kuwa kauli zao ni hatari na zinajenga chuki ndani ya taifa.


Malumbano kati ya wanasiasa hao, yaliibuka baada ya Mwenyekiti huyo mstaafu wa CCM kudai kuwa kwa kipindi chote alichowahi kufanyakazi na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hakuwahi kusikia kama kulikuwa na mwanafamilia anayeitwa Vincent Nyerere.


Juzi, malumbano hayo yalichukua sura mpya  baada mtoto wa kiume wa Mwalimu Nyerere, Madaraka kuibuka na  kuthibitisha kuwa Vincent ni mdogo wao na ni mwanafamilia ya Mwalimu, kwani ni mtoto wa baba yao mdogo, marehemu Josephat Kiboko Nyerere.


Hata hivyo, Madaraka katika majibu yake mafupi kwa Mwananchi aliyoyatuma kwa barua pepe, aliweka wazi kwamba asingependa kujibu maswali mengine zaidi ya kuthibitisha undugu wake na Vincent, akihofu kuingilia kampeni za uchaguzi mdogo wa Arumeru na kushauri maswali mengine yajibiwe na Mkapa mwenyewe au mbunge huyo.  


Tendwa alisema kauli ya Mkapa dhidi ya Vincent na majibu ya mbunge huyo, ni kinyume cha siasa zilizotarajiwa katika uchaguzi huo mdogo ukizingatia kwamba kauli hizo zinakuja katika kipindi cha kampeni, jambo ambalo linaweza kuibua chuki katika taifa na kusababisha vurugu ndani ya jamii.


CHANZO: Gazeti la Mwananchi. SOMA ZAIDI

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII