Mwakyembe aanika ufisadi ATCL
By Maganga Media - Jun 8, 2012
SIKU nne baada ya kung’olewa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameamua kuanika tuhuma za ufisadi zinazodaiwa kufanywa na kigogo huyo.Miongoni mwa tuhuma hizo ni kuingia mkataba wa kununua ndege bila kumhusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na kununua sare 15 za watumishi wa ndege kwa dola 50,000 za Marekani.
Juni 5, Dk Mwakyembe alitengua uteuzi wa Chizi na kumteua rubani wa muda mrefu, Kapteni Lusajo Lazaro kukaimu nafasi hiyo, akisema uteuzi ulikiuka Sheria za Utumishi wa Umma.
Mbali na kutengua uteuzi huo, pia alitangaza kuwasimamisha kazi vigogo wengine wanne wa shirika hilo, hatua ambayo ilianza kuibua malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi kwamba hatua hiyo ilitokana na majungu na ukabila.
Waliosimamishwa kazi na Dk Mwakyembe ni Kaimu Mkurungenzi wa Uhandisi, Jonh Ringo, Mwanasheria ,Amini Mziray, Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Justus Bashara na Josephat Kagirwa ambaye alikuwa Kaimu Mkurugenzi wa Biashara.
Jana, waziri huyo wa uchukuzi aliamua kufafanua tuhuma moja hadi nyingine zinazomhusu kigogo huyo na wenzake na kusema, mbali ya tuhuma za Chizi, wakurugenzi wawili wa shirika hilo walikwenda kushonesha sare 15 za wahudumu wa ndege nchini China kwa gharama ya dola 50,000 za Marekani (karibu Sh80 milioni).
Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo katika Uwanja wa Ndege wa zamani (Terminal One) jijini Dar es Salaam, Dk Mwakyembe alisema kutokana na hali hiyo, ameagiza kujazwa kwa nafasi zilizo wazi na kuwaonya watakaozichukua, kuhakikisha wanachapa kazi ili ATCL ipige hatua na kama wakishindwa watakuwa wamejiondoa wenyewe.
Dk Mwakyembe alitoa miezi mitatu kwa shirika hilo kuanza kujiendesha kwa faida, ikiwa ni pamoja na kupata fedha za kuwalipa wafanyakazi wake.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII