HABARI MPYA LEO  

Mnyika atolewa Bungeni!

By Emmanuel Maganga - Jun 20, 2012


BUNGE jana lilichafuka tena baada ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kusema kuwa Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, kauli ambayo ilisababisha Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru atolewe bungeni.

Mnyika alitoa kauli hiyo wakati akichangia hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2012/13, ambapo alieleza kuwa analazimika kusema Rais Jakaya Kikwete ni dhaifu, wabunge ni wazembe na nchi imefika hapa ilipo kutokana na upuuzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

"Mimi nasikitishwa na jambo moja, tumefika hapa kutokana udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa bunge na wabunge na tumefika hapa kutokana na upuuzi wa CCM, nasema hivi nina ushahidi.”

Lukuvi/ Ndugai
Kauli hiyo ya Mnyika ndio ilichafua hali ya hewa bungeni, ambapo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge na Uratibu, William Lukuvi ndipo alisimama na kuomba mwongozo wa Spika.
“Nataka kumbukusha Mnyika, kutokana na kauli zake, kwa kutumia kanuni ya 64 (d) ambayo inaeleza mbunge yeyote hatatumia jina la Rais kwa dhihaka katika mjadala au kulishawishi bunge kwa jambo lolote,” alisema Lukivi.

Aliendelea kufafanua kuwa, “Lugha kwamba Rais Kikwete ni dhaifu, CCM ni wapuuzi nilikuwa naomba, Mheshimiwa Mnyika, miongoni mwa watu ninaowaheshimu sana, nadhani katika hili, amepotoka naomba afute kauli yake.”
Baada ya kauli hiyo ya Lukuvi, Ndugai alifafanua zaidi kuhusu jambo hilo akisema ni kweli kanuni inajieleza vizuri sio tu katika maneno yake pia amelisema vibaya Bunge hilo na kumtaka afute kauli hiyo.

Mnyika alisimama na kuomba apewe nafasi ya kufafanua kauli yake ya kwanini Kikwete ni Rais dhaifu, lakini Naibu Spika, alimuomba afute kauli yake, kitu ambacho mbunge huyo aligoma kufanya, badala yake akasisitiza bunge limpe nafasi ya kufafanua.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII