HABARI MPYA LEO  

Binti apika bangi badala ya mchicha, Familia yapagawa!

By Emmanuel Maganga - Jun 20, 2012

Msichana wa miaka 16 nchini Kenya amefanya kituko baada ya kukosea na kupika bangi kama mboga kwa ajili ya chakula cha familia jioni huko Kiarimui kwenye wilaya ya Embu.. Standard Media wamesema baba mzazi wa huyo binti ambae ni mwalimu wa sekondari ana shamba nyumbani ambalo lina mboga mbalimbali ambazo huwa zinanawiri wakati wote, kiangazi na vuli.

Jioni hiyo mama wa huyo binti alimuagiza mwanae ambae amerudi nyumbani kwa likizo kwenye kupika ugali na mboga za majani, sasa mtoto alipokwenda shambani kuchukua mboga hakuweza kutofautisha bangi na mchicha.

Sasa noma ikawa kwenye msosi baada ya kuiva ambapo mtoto wa mwisho wa hiyo familia ambae ni wa kiume alianza kucheka kucheka ovyo na ndio alikua wa kwanza wa kupakua msosi mezani, alipomaliza kupeleka matonge mawili akasikia usingizi na kuzimika hapohapo, wengine pia walipakua msosi na kweli na wao wakaanza kucheka cheka ovyo.

Kingine cha ajabu wakati wako mezani kuna mjusi alipita ukutani alafu wote wakaanza kucheka na kutoa machozi baada ya kumuona, stori ilibadilika baada ya baba mwenye nyumba kuanza kumfokea mkewe huku akisema anawapa watoto kazi ambazo sio saizi yao.

Alipoinua mkono kumpiga mkewe na yeye kicheko kikamzidi ambapo kwa mujibu wa huyo mpishi kisa kizima kilianza kuwa kama movie na ikabidi waombe msaada kwa majirani ili kuelewa kilichotokea.

Baadhi ya majirani walifikiri kwamba huenda kuna majini yameipata hiyo familia ila wengine wakasisitiza hao watu wapelekwe kwenye kituo cha afya ambapo baada ya kupimwa damu zao zilikutwa zimejaa sumu ya dawa za kulevya, walitibiwa na kurudi nyumbani ila baba mwenye nyumba anakabiliwa na mashitaka ya kulima bangi shambani kwake.

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII