Anglikan wapinga ndoa za jinsia moja Uingereza!
By Maganga Media - Jun 13, 2012
Kanisa la Kianglikana la nchini Uingereza limepinga vikali mpango wa serikali wa kutaka kuhalalisha ndoa za wapenzi wa jinsia moja. Taarifa rasmi ya kanisa hilo imesema kuwa sheria hiyo iliyopendekezwa imeleta mgawanyiko na ni yenye mapungufu -na inayotishia kuleta Uhasama mkubwa baina ya Kanisa na Serikali.
Mpango wa serikali kutaka kuruhusu ndoa za jinsia moja ifikapo mwaka 2015, huenda ikahujumu maadili ya kanisa la kitaifa. Hata hivyo, taarifa kutoka wizara ya mambo ya ndani zimesema kuwa makanisa hayatashurutishwa kufungisha ndoa za jinsia moja na kwamba serikali itazingatia maoni kutoka pembe zote kabla ya kutunga sheria. Nayo mashirika ya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja wametuhumu kanisa kwa kusambaza uvumi.
Hatua ya Kanisa la England kuelezea wasiwasi kuhusu kutoweka kwa jukumu lake kubwa la kufungisha ndoa na kugusia uwezekano wa kupotoka kwa msingi wake , inalenga kutahadharisha umma juu ya ukubwa wa kile inachoamini ndio pendekezo la sheria kuhusu ndoa za jinsia moja.Inasema kuwa taasisi kama hiyo yenye umuhimu kwa jamii kwa ujumla inahujumiwa ili kuafikia malengo ya kisiasa na inapendekezwa kwa maksudi kama kitu kilicho na umuhimu mkubwa
Maafisa wa kanisa wanadai ikiwa hoja yao ya kutotaka kufungisha ndoa za jinsia moja ingawa hawashurutishwi kufanya hivyo na sheria hiyo, itapelekwa katika mahakama za nyumbani na za nchi wanachama wa Muungano wa Ulaya bila shaka watashindwa.
Waziri wa chama cha Tory Crispin Blunt , alisema kuwa hatua ya serikali kulinda makanisa dhidi ya kufungisha ndoa za jinsia moja huenda ikawa tatizo kisheria. Lakini mapendekezo ambayo serikali inatoa ni kwamba ndoa inapaswa kuwa kati ya wapenzi wa jinsia moja au kati ya mwanamke na mwanaume.
Wakili wa haki za binadamu Lucy Scott-Moncrieff, na ambaye pia ni makamu rais wa chama cha wanasheria,
alisema kuwa mahakama ya muungano wa ulaya ina msimamo mzuri kuhusu maswala yanayoibua hisia tofauti za kidini.Ikiwa swala hilo litapelekwa katika mahakama hiyo, majaji huenda wasikubali kwamba taasisi yoyote ya kidini itaweza kulazimishwa kufungisha ndoa za jinsia moja, lakini akaongeza kuwa kuna baadhi ya makanisa ambayo yangependa kuruhusiwa kufungisha ndoa za jinsi moja.
alisema kuwa mahakama ya muungano wa ulaya ina msimamo mzuri kuhusu maswala yanayoibua hisia tofauti za kidini.Ikiwa swala hilo litapelekwa katika mahakama hiyo, majaji huenda wasikubali kwamba taasisi yoyote ya kidini itaweza kulazimishwa kufungisha ndoa za jinsia moja, lakini akaongeza kuwa kuna baadhi ya makanisa ambayo yangependa kuruhusiwa kufungisha ndoa za jinsi moja.
Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS
ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII