HABARI MPYA LEO  

AJARI YA BASI TABORA

By Maganga Media - May 3, 2012

WATU saba wamekufa na wengine 54 kujeruhiwa vibaya katika ajali ya basi iliyotokea jana wilayani Igunga, Tabora.Habari zilisema ajali hiyo iliyohusisha basi la Kampuni ya NBS ilitokana na kupasuka kwa tairi moja la mbele na hivyo kusababisha gari kupinduka.

Kwa mujibu wa baadhi ya watu walioshuhuda, ajali hiyo ilitokea mapema asubuhi mjini Igunga wakati basi hilo likitoka Tabora kwenda Arusha.Walisema maiti na majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.

Mganga mfawidhi  wa hiyo, Dk Godfrey Kissila, alithibitisha kupokelewa na kuhifadhiwa kwa maiti za watu waliokufa katika tukio hilo."Maiti hao ni za wanawake watatu, wanaume watatu na mtoto mmoja," alisema mganga huyo.

Alisema majeruhi wapatao 54 wamelazwa katika hospitali hiyo na kwamba saba miongoni mwao hali zao ni mbaya.Mara baada ya ajali hiyo, magari ya maalumu ya kubebea wagonjwa, yalikwenda katika eneo la tukio na kufanyakazi ya kubeba majeruhi na kuwapeleka katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga.

Katika hospitali hiyo, waganga na wauguzi walionekana wakishirikiana kujaribu kuokoa maisha ya majeruhi

Follow Maganga Media on Twitter, Feel free to like and comment Facebook. Stay updated via RSS

ANDIKA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII